Ni kauli ya sheria ambayo inatumika karibu kwenye kila eneo la maisha yetu.
Usipofanya kitu kwa sababu hujui usifikiri asili itakuacha salama. Lazima itakupa adhabu ya kutokujua kwako, kwa mfano, unavunja sheria kwa sababu ya ujinga wa kutokujua sheria, usifikiri kutokujua kwako kunaweza kukusaidia, hapana.
Angalia sheria za asili zinavyofanya kazi. Watu hawajui misingi ya maisha, fedha, biashara na mafanikio kiujumla lakini ulishawahi kuona asili inawaacha? Asili ina adhibu watu bila kujali, kama hujui basi utajifunza kwa makosa na utalipa riba mkusanyiko uwe unataka au la.
Matatizo ya kifedha hayajawahi kuisha yote hii ni kwa sababu watu hawataki kuishi misingi ya fedha. Na kutokujua misingi ya kifedha siyo msamaha wa wewe kutokuadhibiwa. Ona watu wanatapeliwa kila siku, madeni, kukosa fedha, matumizi yasiyokuwa na ulazima, kuishi juu ya kipato.
Kwenye maisha yako usiwe na kisingizio, ingia na weka kazi kwenye kile unachotaka na utakipata kweli. Kama unanufaika na kujifariji kwa mdomo endelea kufanya hivyo lakini kama unaona maisha yako hayakupi kile unachotaka, wewe ndiyo dereva badilisha gia.
Pambana mpaka ufikie kile unachotaka, acha kujipa sababu kwa sababu, sababu hazilipi bili. Kama ulishawahi kwenda dukani na ukanunua kitu kwa sababu basi endelea nayo.
Usijipe sababu, tafuta matokeo tu. Wewe weka kazi kweli bila kumdanganya mtu na asili itakupa matokeo mazuri, asili itaendelea kukuadhibu kwa sababu ya kuidanganya. Tafadhali, huna unayemdanganya, kumbuka mtu wa kwanza kukuona ni wewe mwenyewe.
Usipotimiza wajibu wako vizuri kwenye kila eneo la maisha yako, asili haitokuacha salama. Timiza wajibu wako vizuri kwenye kazi, biashara, familia, ndoa, huduma nk.
Kuwa vizuri kiroho, kiakili na kimwili kwani ni vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako.
Hatua ya kuchukua leo;
Kama hujui kitu jifunze na usitumie kigezo cha kutokujua kwako kama sababu ya wewe kutokufanikiwa.
Hivyo basi, Usipojifunza na kuchukua hatua dunia itaendelea kukuadhibu mpaka pale utakapobadilika.
Na maneno hayajawahi kukamilisha kitu, kama unataka kutokea kwenye historia ya dunia pambana na weka kazi kweli.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog