Design a site like this with WordPress.com
Get started

Rudia Tena Kufanya

Karibu kila mtanzania anajua kuimba wimbo wa Taifa bila shida yoyote ile. Na watu wanaweza kuimba wimbo wa Taifa kwa sababu walivyokuwa shuleni walikuwa wanauimba karibu kila siku. Hii imepelekea hata watu wengi kuunasa kichwani na kuuelewa bila shida.

Hapa tunajifunza kitu kikubwa sana, ukitaka watu wakielewe kitu, unapaswa kukirudia rudia kitu mara kwa mara ndiyo akili inashika.

Ukitaka ukielewe kitabu, kisome na kirudie tena na tena mpaka ukielewe. Chochote ambacho unataka kinase kwenye akili na ukielewe vizuri, usifanye mara moja bali rudia mara nyingi.

Kwa mfano, watoto wengi wana uwezo wa kushika nyimbo mbalimbali za wasanii na kuimba bila shida lakini ukija kwenye masomo ya darasani hawashiki, hii ni kwa sababu nyimbo huwa wanaisikiliza mara kwa mara, inajirudia kwenye akili yao na kutengeneza kumbukumbu ya kudumu.

Ukitaka watu wakielewe kitu, rudia mara kwa mara kile wanachotaka kuelewa. Usifanye mara moja na kusema basi, ila rudia tena kufanya.

Huwezi kuona matokeo mazuri kwa kufanya kitu mara moja, ila kwa kurudia rudia mara kwa mara inakusaidia kuwa bora.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka uelewe kitu usifanye mara moja bali kirudie mara kwa mara ndiyo kitakaa kichwani.

Vitabu vyote ulivyosoma virudie tena kuvisoma. Masomo mazuri uliyowahi kuyapata iwe ni semina, makala zirudie, kusoma mara moja haitoshi bali rudia tena mpaka akili izoee na kupata uelewa mzuri.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: