Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mafanikio Mengi Ya Kifedha Huwa Yanakuja Na Hili Pia

Mwanamziki wa kimarekani Rick Ross kwenye moja ya wimbo wake mmoja anasema fedha nyingi, matatizo mengi, usiniite bosi yaani more money, more problem don’t call me the boss.

Mafanikio ya kifedha huwa yanakuja na matatizo makubwa ya kifedha pia.

Siyo kwamba ukishakuwa na fedha nyingi ndiyo umeshayapatia maisha yako, yaani huhitaji tena kuhangaika hapana, siyo kweli.

Kwa mfano, Juma huwa anapata kipato chake kwa mwezi milioni 10 na Anna huwa anapata kipato chake kwa mwezi milioni moja.
Kwa mfano huo hapo, unaweza kuona Juma hana shida kabisa ila Ana ndiyo ana shida sana maana kipato chake ni kidogo. Kumbe, jua kipato chake ni kikubwa kwa mwezi lakini matatizo anayotatua ni makubwa pia. Kwahiyo, yule mwenye kipato kikubwa anakuwa na matatizo makubwa yanayohitaji kutatuliwa na fedha ukilinganisha na mtu ambaye kipato chake ni kidogo kabisa.

Ndiyo maana mtu akishakuwa na fedha huwa anaongeza juhudi kupata zaidi kwa sababu anajua kadiri unavyofanikiwa kifedha ndivyo unavyozidi kukaribisha matatizo mengi pia.

Kuna picha ambayo tayari imejengeka kwamba mtu akishakuwa na fedha nyingi basi yeye hana matatizo tena wala hahitaji kuhangaika tena.

Utawasikia mpaka watu wengine wanasema mtu ana fedha nyingi lakini bado anahangaika tu, ingekuwa mimi ningelala na kula bata(raha) tu.

Usiwe na fikra kama hizo za kimasikini kwa sababu ndizo zinawafanya watu wengi kuendelea kuwa masikini.

Unapokuwa na fedha nyingi, kila mtu anakuwa anafikiria namna ya kupata fedha zako. Wengine wanafikiria namna wanavyoweza kukuibia au kukutapeli, bado wale ambao watajenga mahusiano na wewe lakini siyo mahusiano ya kweli lakini lengo lao kubwa ni kunufaika na fedha zako.

Bado kuna changamoto nyingi kama vile za kazi, biashara unayofanya. Kwahiyo, kadiri unavyokuwa kifedha ndivyo fursa za kupoteza fedha zinavyozidi kuwa kubwa.

Hatua ya kuchukua leo; Jiandae kupata fedha nyingi lakini usisahau pia fedha nyingi huja na matatizo makubwa pia.

Hivyo jiandae,” kama milioni moja inakutoa jasho, jua milioni kumi zitakutoa machozi na huenda milioni mia zikakutoa damu”

Usishangazwe na hili, mtu ambaye ana fuga kuku kumi, hawezi kuwa sawa na mtu ambaye anafuga kuku mia katika kutatua changamoto za kuku kifedha.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: