Mbinu Mbili Za Kumshawishi Mtu Aliyekuzidi

Kuna wakati unataka kumshawishi mtu aweze kukubaliana na wewe lakini unajikuta unashindwa kufanya zoezi hilo labda kwa kuona yule unayetaka kumshawishi amekuzidi karibu kila kitu. Sasa kama mtu ameshakuzidi kwa kila kitu wewe utamwambia nini sasa? Kama ulikuwa na tatizo kama hilo, leo nakwenda kukupatia suluhisho lako. Pata picha kwamba unaenda kumshawishi mtu aliyekuzidi na …

Utajisikiaje kama Ukikosa Kupata Maarifa Haya

Habari njema kwako rafiki yangu, Pata picha mtu anavyokuwa anateseka na kupata maumivu ya ndani pale wanapokuwa wametofautina na rafiki, ndugu, jamaa au watu wa karibu. Nadhani unapata picha ya maumivu ambayo mtu anakuwa nayo pale anapokuwa ameumizwa na mwingine kwa namna yoyote ile? Utajisikiaje kama unaishi na majeraha ya nafsi huku aliyekujeruhi wala hana …

Vitu Unavyopaswa Kuacha Mara Moja Kama Unataka Kuwa Na Furaha

Viko vitu vingi sana vinavyowafanya watu wasiwe na furaha, lakini mimi leo nitakushirikisha kitu kimoja tu. Kama unataka kuwa na furaha, acha kitu hiki.USIPOTEZE MUDA WAKO KWENYE VITU AMBAVYO HUWEZI KUVIDHIBITI Kwenye maisha tunayo makundi ya aina mbili. Moja, vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako. Hivi ni vile vitu ambavyo unaweza kuvibadili kwa sababu …

Inafanya Kazi Vizuri Sana

Kabla mteja hajanunua kitu kwako anachotaka ni kupata uhakika juu ya kile unachouza kwanza. Sasa wauzaji wengi huwa hawawapi wateja uhakika. Hata mgonjwa akiwa anaumwa akimuuliza daktari je, nitapona na daktari akimpa matumaini ndiyo utapona mgonjwa anakuwa na matumaini lakini akimwambia huponi atampoteza. Na unaweza kumpoteza mteja kama hujampa uhakika wa kile unachouza. Ukimwambia hakifanyi …

Haya Ndiyo Maisha Ambayo Hayana Maana Kuishi

Ni maisha ambayo hayatathiminiwi. Mwanafalsafa Socrates aliwahi kunukuliwa akisema, maisha ambayo hayatathiminiwi, hayana maana kuishi. Watu wengi hawajifanyii tathimini kwenye kile wanachofanya ndiyo maana hawaoni matokeo mazuri, hawajui kama wanaenda mbele au wanarudi nyuma. Fanyia tathmini kazi yako. Jiulize kazi unayofanya inakulipa? Na itakufikisha kweli kule unakotaka kufika?Kazi unayofanya inasaidia jamii au ina haribu maisha …

Jinsi Ya Kula Mema Ya Nchi

Kila mtu amepewa kibali cha kula mema ya nchi. Kila mtu amebarikiwa kwenye maisha yake. Unachopaswa kujua ni kwamba, baraka huwa haziji tu kwako bila kufanya kitu. Baraka huwa zinakuja kwako kwa kufanya kitu. Ukifanya kitu na utaona baraka zinakuja. Baraka haziji kwa kuweka mikono mifukoni, bali baraka zinakuja kwa kufanya kitu. Ili uweze kuchota …

Biashara Mpya Ambayo Haijawahi Kufanywa Na Mtu Yeyote Yule Na Ina Fursa Nyingi Kweli

Kifupi tu rafiki yangu, hakuna biashara mpya ambayo haijawahi kufanywa. Biashara ni zile zile lakini tatizo liko kwenye utoaji wa huduma. Unaweza ukafanya biashara yako kuwa mpya kwa kuifanya ya kipekee sana kuliko nyingine zote ambazo tayari zilikuwepo. Usipate shida kutafuta wazo la biashara, unachotakiwa kufanya angalia biashara ambazo ziko mtaani kwako au changamoto ambayo …

Kadiri Unavyoweka Juhudi Za Kuongeza Kipato, Kuwa Makini Na Matumizi Yako

Fedha ikiwepo huwa haikosi matumizi. Unapokuwa na fedha mara nyingi inatafuta matumizi na sasa usipokuwa makini utajikuta huna unachofanya. Lazima uwe mjanja, kwani kuna kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato chako kinapoongezeka. Ukitaka uione hela, ongeza kipato chako na punguza matumizi yasiyokuwa na ulazima. Usipokuwa makini na matumizi, utashangaa mwanzoni ulikuwa na kipato kidogo na …

Bila Ya Kuwa Na Kitu Hiki Huwezi Kufanikiwa Kwenye Maisha

Katika safari ya mafanikio ya kuyafikia mafanikio makubwa inahitaji mtu mwenye sifa kuu mbili, kwanza mtu ambaye anajituma na kujiongoza. Bila ya kuwa mtu wa kujituma wewe mwenyewe, ni vigumu kufanikiwa kwenye maisha. Wapo watu ambao wanasubiri kuambiwa cha kufanya, bila kuambiwa hawajisumbui kabisa kifupi wanakosa nidhamu binafsi. Lakini wale wanaofanikiwa sana huwa hawasubiri kuambiwa …

Tengeneza Maoni Yatakayokupa Hamasa Binafsi

Yapo maoni mengi ambayo huwa tunajitengenezea kwenye fikra zetu. Yapo maoni ambayo tunajipa sisi wenyewe na yapo maoni ambayo yanajitengenezea kwenye fikra zetu. Wako ambao wanajipa maoni chanya na wako ambao wanajipa maoni hasi. Maoni yanayotengenezwa kwenye fikra zetu yana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu kimaisha. Kujitengenezea maoni ni hamasa binafsi. Vile unavyofikiri upo …

Design a site like this with WordPress.com
Get started