Kabla mteja hajanunua kitu kwako anachotaka ni kupata uhakika juu ya kile unachouza kwanza.
Sasa wauzaji wengi huwa hawawapi wateja uhakika. Hata mgonjwa akiwa anaumwa akimuuliza daktari je, nitapona na daktari akimpa matumaini ndiyo utapona mgonjwa anakuwa na matumaini lakini akimwambia huponi atampoteza.
Na unaweza kumpoteza mteja kama hujampa uhakika wa kile unachouza. Ukimwambia hakifanyi kazi vizuri ataacha kukinunua.
Kama unataka kumshawishi mteja akubaliane na wewe juu ya bidhaa unayouza akikuuliza inafanyaje kazi, mjibu inafanya kazi vizuri sana au inafanya kazi kwa ubora wa hali ya juu.
Wanachotaka watu ni uhakika tu, hivyo unapotaka kufanya mauzo, hakikisha unamwakikishia mteja uhakika.
Hatua ya kuchukua leo; Kama unashindwa kuielezea bidhaa au kile unachouza, wewe sema tu hii inafanya kazi vizuri sana ni maneno ambayo mtu akiyasikia atapata uhakika.
Wape watu uhakika juu ya kile unachouza, ukitaka ufanye mauzo na mteja akija kwako asiondoke bila kununua tumia maneno yenye nguvu ya ushawishi.
Si unajua watu ni wagumu kujitenganisha na fedha zao, hivyo ukimwakikishia kwamba kile unachomuuzia ni kizuri na kitakwenda kumsaidia, basi atashawishika kununua.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog