Fedha ikiwepo huwa haikosi matumizi. Unapokuwa na fedha mara nyingi inatafuta matumizi na sasa usipokuwa makini utajikuta huna unachofanya.
Lazima uwe mjanja, kwani kuna kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato chako kinapoongezeka.
Ukitaka uione hela, ongeza kipato chako na punguza matumizi yasiyokuwa na ulazima.
Usipokuwa makini na matumizi, utashangaa mwanzoni ulikuwa na kipato kidogo na mambo yalikuwa yanaenda vizuri, lakini leo kipato chako kimeongezeka na matumizi nayo yanaongezeka.
Kipato kikiongezeka, na wewe usiongezeke kwenye matumizi, ishi maisha yako kama ulivyokuwa unaishi na utaweza kuiona fedha.
Matumizi hayajawahi kuisha, ukiwa na fedha matumizi yanakuja yenyewe. Usikubali fedha ikutawale, wewe ndiyo uitawale fedha.
Yako matumizi ya aina mbili, moja matumizi yasiyokuwa na ulazima na yale yenye ulazima.
Kuna matumizi yasiyokuwa na ulazima, unaweza ukayaepuka na maisha yakaendelea lakini kuna matumizi ya lazima, lazima ufanye ili maisha yako yaende vizuri. Kuna matumizi usipofanya maisha yako hayawezi kwenda mbele.
Hatua ya kuchukua leo; Kuwa makini na matumizi yasiyokuwa na ulazima.
Ishi maisha yako kwa kutumia kidogo na kuongeza kipato zaidi.
Kwa kutumia kanuni hii, ya kuongeza kipato na kupunguza matumizi yasiyokuwa na ulazima kwenye maisha yako utaweza kuiona hela.
Ukishaiona hela utaweza sasa kufanya uwekezaji ambao utakusaidia kuzalisha fedha zaidi.
Utajiri ni pale fedha inapokufanyia kazi wewe na siyo wewe kuifanyia kazi fedha. Pata fedha iwekeze na usikimbilie tu kutumia maana utaishia kuwa mtu wa kuitumikia fedha badala fedha ikutumikie wewe.
Wekeza ili ununue uhuru wako mapema, maisha ni uhuru tumia kila fedha unayopata kwa nidhamu kwani unaipata kwa shida kwanini sasa unakubali kuipoteza kirahisi.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog