Jinsi Ya Kula Mema Ya Nchi

Kila mtu amepewa kibali cha kula mema ya nchi. Kila mtu amebarikiwa kwenye maisha yake.

Unachopaswa kujua ni kwamba, baraka huwa haziji tu kwako bila kufanya kitu. Baraka huwa zinakuja kwako kwa kufanya kitu.

Ukifanya kitu na utaona baraka zinakuja. Baraka haziji kwa kuweka mikono mifukoni, bali baraka zinakuja kwa kufanya kitu.

Ili uweze kuchota baraka,unapaswa ufanye kitu kwanza. Kwa mfano, mzazi huwa anachilia baraka kwa mtoto pale mtoto anapokuwa anamfanyia kitu ambacho kimempendeza na kamwe mzazi hawezi kuachilia baraka kwa mtoto ambaye hata hajitumi wala kuonesha juhudi yoyote ile.

Je, unakulaje sasa mema ya nchi?

Ukitaka kula mema ya nchi, basi toa thamani kubwa kwa wengine.

Njia ya kutoa thamani kwa wengine ndiyo njia ambayo itakuwezesha wewe kula mema ya nchi. Kupitia kutoa thamani kubwa kwa wengine utapata kile unachotaka.

Hakuna juhudi yoyote unayoweka halafu ikaenda bure, hivyo unapowawezesha wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka. Na ukishapata kile unachotaka utakua umekula mema ya nchi.

Mema ya Nchi yapo kwa wale wanaojitoa kutafuta kile wanachotaka na kamwe usitegemee kula mema ya nchi kama hujitoi kutoa thamani kwa wengine.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kula mema ya Nchi, nenda katoe thamani au mchango wako kwa wengine.

Ukitaka kufanikiwa kwenye maisha, wawezeshe watu wengi zaidi kupata kile wanachotaka na wewe pia utapata kile unachotaka kwenye maisha yako.

Hii ni kanuni ya asili, ukiifuata lazima utakula mema ya nchi mpaka ushangae.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started