Yapo maoni mengi ambayo huwa tunajitengenezea kwenye fikra zetu.
Yapo maoni ambayo tunajipa sisi wenyewe na yapo maoni ambayo yanajitengenezea kwenye fikra zetu.
Wako ambao wanajipa maoni chanya na wako ambao wanajipa maoni hasi.
Maoni yanayotengenezwa kwenye fikra zetu yana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu kimaisha.
Kujitengenezea maoni ni hamasa binafsi. Vile unavyofikiri upo na kile unachojiambia kila mara ndiyo kinachotokea kwenye maisha yako.
Unapokuwa mtu wa kujitengenezea maoni mazuri ya mafanikio makubwa, ndivyo unavyohamasika kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; Tengeneza maoni kwenye fikra zako yatakayokuhamasisha kupiga hatua zaidi kwenye kile unachofanya.
Maoni binafsi yako ndani ya uwezo wako, usisubiri mpaka upewe maoni na watu wengine. Anza kujitengenezea maoni mazuri yenye hamasa.
Kutengeneza maoni ni bure, usiache kuwa na maoni chanya juu yako mwenyewe.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog