Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mbinu Mbili Za Kumshawishi Mtu Aliyekuzidi

Kuna wakati unataka kumshawishi mtu aweze kukubaliana na wewe lakini unajikuta unashindwa kufanya zoezi hilo labda kwa kuona yule unayetaka kumshawishi amekuzidi karibu kila kitu.

Sasa kama mtu ameshakuzidi kwa kila kitu wewe utamwambia nini sasa?

Kama ulikuwa na tatizo kama hilo, leo nakwenda kukupatia suluhisho lako. Pata picha kwamba unaenda kumshawishi mtu aliyekuzidi na anakubaliana na wewe kwa mbinu hizi mbili ninazokwenda kukushirikisha hapa.

Binadamu wote ni viumbe vya hisia, ukiweza kuzijua hisia za mtu ziko wapi na kuzigusa ni rahisi sana kumshawishi na kukubaliana naye awe amekuzidi au la.

Kwa sababu watu wengi huwa wanafanya maamuzi kwa hisia na kuja kuhalalisha kwa kufikiri.

Mbinu ya kwanza, tengeneza ukaribu ambao unaongeza ushawishi kwa watu hao. Watu huwa wanapenda kuona kuwa uko upande wao. Anza kutengeneza kwanza ukaribu ambao unaongeza ushawishi kwa mtu huyo. Watu wakiona unafanya kile ambacho yeye anafanya au anapenda anaanza kuona wewe ni mwenzake.

Hata ukiwa kwenye maongezi jaribu kumsoma yule unayeongea naye, maneno anayopendelea kuyatumia mara kwa mara yaani individuality yale maneno ya upekee kwenye lugha ambayo mtu anapendelea kuyatumia sana na kuyarudia na wewe yatumie ukiwa naye.

Angalia pia namna anavyokaa, igiza kile anachofanya lakini asigundue kwa mfano, kama unakutana naye anapendelea kukaa akiweka nne na wewe kunja nne.

Mara nyingi watu wanashawishika pale unapokuwa upande wao kwa kufanya vile vitu ambavyo wao wanapenda.

Pili wape watu zawadi. Watu wanapenda zawadi na wanathamini sana vitu ambavyo wanapewa na watu, ukimpa mtu zawadi hata kama ni ndogo kiasi gani ataendelea kuikumbuka na kuithamini.

Nikupe siri moja, watu wengi wanapenda kupokea hata kama wana kila kitu.

Jaribu kucheza na hisia za mtu huyo, kamata umakini wake, jua nini anapendelea zaidi na mnunulie zawadi ya kile anachopenda. Kwa mfano, labda mtu huyo unayetaka kumshawishi amekuzidi na unajua labda ni shabiki wa timu fulani, unachotakiwa kufanya ni wewe kwenda kununua jezi ya timu hiyo na kuandika jina lake.

Hakuna kitu ambacho watu wengi wanapewa kama majina yao, halafu jina lake umeliandika kwenye kitu ambacho unakipenda.

Baada ya kutumia mbinu hizo na utakua umeshamteka sasa pale pale anapokuwa kwenye kilele cha furaha au hisia kuwa juu, mshawishi kwenye kile unachotaka sasa aweze kukubaliana na wewe.

Mbinu hii unaweza kuitumia hata kwa wateja wako, ukishajua wateja wako wanapenda nini, ni rahisi kuwashawishi na kununua kile unachouza.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kumteka mtu kwenye kitu chochote kile na kuweza kukubaliana na wewe kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kucheza na hisia zake tu.

Kumbuka watu wanafanya maamuzi kwa hisia, hivyo ukiweza kugusa hisia zao utaweza kuwashawishi na kukubaliana na wewe.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: