Mpendwa rafiki yangu,
Heri ya mwezi machi,natumaini unaendelea vema kuwa bora kila siku na kuhakikisha unafikia malengo yako.
Sisi binadamu wote tuko katika mwendo, kwanza tokea unazaliwa moyo wako haujawahi kusimama kufanya kazi hivyo siku utakaposima na wewe ndiyo utakua mwisho wako hapa duniani.
Miili yetu kiasili iko katika mwendo. Kila kitu kipo katika mwendo, ukiacha kuwajibika hutoweza kujikimu katika maisha hivyo basi kiasili yetu ni mwendo.
Mwandishi na mwanafalsafa Ryan Holiday aliwahi kunukuliwa akisema, sheria kubwa ya asili ni ile inayosema kamwe usisimame. Hakuna mwisho.
Ninakubaliana kabisa na Holiday kwa sababu dunia yenye iko katika mzunguko ndiyo maana tunapata usiku na mchana. Tokea Mungu aiumbe hii dunia haijawahi kusimama hata siku moja. Hivyo , na sisi hatupaswi kusimama kwenye eneo lolote la maisha yetu.
Kila kitu kinatutaka tusiache kufanya, tusisimame, tuendelee na mwendo kwa sababu hakuna mwisho.
Ukija katika upande wa fedha, fedha hazina mwisho huwezi kusema kwa sasa nimefikia ukomo wa pesa, namba hazina mwisho hivyo unaweza kuendelea kadiri unavyopenda wewe.
Chochote unachotaka kufanya zaidi bado nafasi ya kuwa bora iko, kwa sababu hakuna mwisho. Unaweza kujiboresha kwenye kila eneo la maisha yako na kuwa bora.
Usiseme nimefika mwisho, eti usimame, bali endelea. Kwa mfano, angalia wale ambao wanasema wamestaafu kufanya kazi na maisha yao yakoje, haiwachuki muda wanaanguka vibaya. Kila kitu kinahitajika kufanyika bila kusimama.
Hatua ya kuchukua leo; usijiwekee ukomo kwenye maisha yako, usisimame kwani asili yenyewe haisimami na inaendelea hakuna mwisho.
Kwahiyo, sheria kubwa ya asili inatuambia kuwa kamwe tusisimame, hakuna mwisho. Tuendelee kupiga kazi na kupambana mpaka tupate kile tunachotaka.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com
Asante sana