Imani Ulizonazo Zinachangia Sana Wewe Kuwa Hivyo Ulivyo

Imani ulizonazo, zinachangia sana kwenye matatizo na changamoto unazokutana nazo. Na ubaya wa imani ni kwamba, mtu unaweza hata usijue kama ni imani iliyopo ndani yako hasa kama ni kitu ambacho umezoea kukifanya. Unahitaji kubadili imani yako juu yako mwenyewe na kile unachokutana nacho. Inawezekana kabisa imani uliyonayo ndiyo inakufanya uende mbele au urudi nyuma. …

Ili Usiwe Tegemezi Kwa Wengine Fanya Hivi

Ili usiwe tegemezi kwa wengine lazima uwe na mengi ndani yako lakini pia, lazima ujue kilichopo ndani yako na uweze kukitumia vizuri. Watu wengi wamekuwa tegemezi kwa wengine, wamekuwa watumwa kwa wengine kwa sababu wamejitelekeza wao wenyewe. Usipojitumia vizuri na kutumia rasilimali ambazo unazo tayari utaishia kuwa tegemezi kwenye maisha yako yote. Unakuwa tegemezi kwa …

Usiwe Na Wasiwasi

Mara nyingi kinachowazuia watu kufanya maamuzi kwenye maisha yao ni wasiwasi wanaokuwa nao juu ya kitu fulani. Kitendo cha watu kuwa na wasiwasi, kinawafanya wasifanye maamuzi kwa kuona bado hawajawa na uhakika wa kutosha. Rafiki yangu, niko hapa kukuondoa wasiwasi, usiwe na wasiwasi juu ya kitu fulani unachotaka kuanza kwenye maisha yako. Usiwe na wasiwasi …

Yote Uliyojifunza Hayatawezekana Kama Utakosa Kitu Hiki Kimoja

Kitu hicho ni uaminifu. Uaminifu ni msingi muhimu sana. Yote tuliyojifunza hapa na tunayoendelea kujifunza hapa hayatawezekana kama utakosa kitu kimoja ambacho ni uaminifu. Unahitaji kuwa na uaminifu wa hali ya juu sana. Wakati mwingine uaminifu wako utakukosesha wateja, hasa pale utakapowaeleza ukweli kwamba kile wanachohitaji hasa wewe huna. Ni bora useme ukweli kuliko kudanganya, …

Kila Wakati Kuwa Na Kitu Hiki

Kuwa na kitu cha kufanyia kazi. Kila wakati kuwa na namba ambayo unapaswa kuifanyia kazi. Usikubali kuwa na maisha ambayo unakuwa na muda halafu huna kitu cha kufanyia kazi. Kila wakati jipe kazi, jipe jukumu moja la kufanyia kazi na ukilimaliza jipe jukumu lingine tena. Hakuna kupoa, ni kazi kazi. Siyo kwamba usiwe na muda …

Tahadhari; Ijue Sheria Ya Mafanikio Kabla Hujapata Anguko

Waandishi Al Ries na Jack Trout kwenye kitabu chao cha THE 22 IMMUTABLE LAWS OF MARKETING wanaelezea sheria za masoko ni namna gani watu wakishapata mafanikio makubwa wanajisahau na baadaye kupata anguko. Maisha ni mauzo yaani kifupi kila kitu kwenye maisha ni mauzo sasa ili uendelee kubaki kwenye mauzo mazuri unapaswa kuwa na masoko endelevu. …

Usichukie Mafanikio Ya Wengine

Ukiona mtu anachukia mafanikio ya wengine jua kabisa hajui maana ya mafanikio kwake ni nini. Mafanikio kwako yana maana gani?Ukishajua mafanikio kwako yana maana gani huwezi kuchukia mafanikio ya watu wengine. Mafanikio yana maana tofauti tofauti kwa kila mmoja wetu. Kwa kulijua hilo usichukie mafanikio ya watu wengine bali yapende. Hakuna kitu kinawazuia watu kufanikiwa …

Usikubali Anayekuonea Aendelee Na Uonevu Wake

Kwenye maisha yako unapaswa kuwa mtu imara. Usipokuwa imara utawaruhusu watu wengine wakutawale na huwezi kuwa huru kwenye maisha yako kama umetawaliwa na mtu fulani. Kwenye maisha yako usiwe mnyonge kabisa, jiamini, na simamia kile unachokiamini. Kama unaishi bila kuvunja sheria za asili, nchi na kanuni za maadili huna cha kuhofia. Bali ishi kwa uhuru …

Tafakari Ya Kumbukizi Yangu Ya Kuzaliwa, Kitabu Kipya; SHOW ME THE WAY, NIONESHE NJIA NA ZAWADI

NAJIWASHA MOTO NJOONI MNIONE NIKIUNGUA Habari rafiki yangu nikupendaye, Leo Julai 18, ninaadhimisha kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa hapa duniani. Nilizaliwa miaka 33 iliyopita. Kwa namna ya pekee kabisa namshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha kwa kunistahilisha kusimama mbele yake na kuendelea kumtumikia na hatimaye leo naadhimisha kumbukumbu yangu ya kuzaliwa. Mwaka jana nilifanya …

Matashi Mema Aliyoniandikia Rafiki Yangu Kwenye Kumbukumbu Ya Kuzaliwa Kwangu

Rafiki yangu, Leo ni siku yangu ya kuzaliwa, katika maamuzi magumu ambayo nimewahi kufanya kwenye maisha yangu mwaka huu basi ni kuachana na ajira. Ni maamuzi sahihi kwangu na leo nayafurahia, sijui nilipata wapi nguvu hiyo lakini namshukuru sana Mungu kwa kunipa nguvu za ajabu za kuachana na ajira. Huwa nafanya sana tafakari ya maisha …

Design a site like this with WordPress.com
Get started