Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiwe Na Wasiwasi

Mara nyingi kinachowazuia watu kufanya maamuzi kwenye maisha yao ni wasiwasi wanaokuwa nao juu ya kitu fulani.

Kitendo cha watu kuwa na wasiwasi, kinawafanya wasifanye maamuzi kwa kuona bado hawajawa na uhakika wa kutosha.

Rafiki yangu, niko hapa kukuondoa wasiwasi, usiwe na wasiwasi juu ya kitu fulani unachotaka kuanza kwenye maisha yako.

Usiwe na wasiwasi kwenye maisha mapya unayotaka kuanza kuishi.

Usiwe na wasiwasi kama unataka kuanza biashara.

Usiwe na wasiwasi kama unataka kuacha kazi ya kuajiriwa na kuanza kujiajiri, kabla hujafanya maamuzi ya kuacha hakikisha tayari umeshakuwa na kitu cha uhakika cha kwenda kufanya pembeni ukiwa nje ya ajira na uwe na akiba angalau ya miezi sita ya kipato chako unachopata kila mwezi.

Usiwe na wasiwasi maisha yako yatabadilika sana ikiwa utazingatia kufanya misingi yote sahihi unayopaswa kufanya.

Najua una mawazo mazuri lakini una hofu ya kuanza. Kuna vitu vingi ambavyo unavihitaji kwenye maisha yako lakini una wasiwasi je, utavipata kweli?

Usiwe na wasiwasi utavipata kweli, kikubwa ni wewe kukaa kwenye mchakato sahihi na matokeo mazuri yatakuja yenyewe baadaye.

Hatua ya kuchukua leo; usiwe na wasiwasi utafanikiwa kwenye kile unachotaka, je, juhudi unazoweka kwenye kazi au biashara zinatosha kweli kukufikisha kule unakotaka kufika?

Kitu kimoja cha mwisho, usiwe na wasiwasi kwa sababu kila ambaye unamuona leo yuko vizuri naye alipitia hali ngumu mwanzoni.
Kila unayemwona yuko vizuri sana kwenye kitu fulani jua naye mwanzoni alikuwa hajui kitu.

Usiwe na wasiwasi kila kitu kinawezekana, usikubali kuamini msamiati wa neno haiwezekani kwenye maisha yako, kwani ni neno linalopatikana kwenye kamusi ya mpumbavu tu, usiwe na wasiwasi wewe ni mtu mwenye bahati sana na wewe ni mshindi na umezaliwa kushinda na maisha yako yamebarikiwa sana.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: