Ili usiwe tegemezi kwa wengine lazima uwe na mengi ndani yako lakini pia, lazima ujue kilichopo ndani yako na uweze kukitumia vizuri.
Watu wengi wamekuwa tegemezi kwa wengine, wamekuwa watumwa kwa wengine kwa sababu wamejitelekeza wao wenyewe.
Usipojitumia vizuri na kutumia rasilimali ambazo unazo tayari utaishia kuwa tegemezi kwenye maisha yako yote.
Unakuwa tegemezi kwa sababu umeacha kuangalia kile kilichopo ndani yako na kukitumia badala yake unahangaika na vile vilivyo kwa wengine.
Kama unatumia vizuri sana akili yako huwezi kuwa mtumwa wa yeyote yule.
Hatua ya kuchukua leo; jijue wewe mwenyewe na kua kilichopo ndani yako na kukitumia vizuri.
Kabla hujajisumbua kutafuta vile ambavyo hauna, hakikisha unavitumia vizuri sana vile ambavyo unavyo.
Kuwa bora kwenye kile unachofanya kiasi kwamba hakuna atakayeweza kukupuuza.
Ukishindwa kujitumikia lazima utatumikishwa.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog