Imani ulizonazo, zinachangia sana kwenye matatizo na changamoto unazokutana nazo.
Na ubaya wa imani ni kwamba, mtu unaweza hata usijue kama ni imani iliyopo ndani yako hasa kama ni kitu ambacho umezoea kukifanya.
Unahitaji kubadili imani yako juu yako mwenyewe na kile unachokutana nacho.
Inawezekana kabisa imani uliyonayo ndiyo inakufanya uende mbele au urudi nyuma. Tafakari kwenye hili na utaona uhalisia wa mambo.
Mambo mengi unayojiambia huwezi siyo kweli kwamba huwezi, ila hujawahi kujaribu kufanya.
Kuwa mtu wa kujaribu na utavuka changamoto nyingi, usikubali imani uliyokuwa nayo ikurudishe nyuma bali imani ulizonazo zinatakiwa zikusukume kwenda mbele.
Hatua ya kuchukua leo; jiulize ni imani zipi ulizonazo kwenye kila eneo la maisha yako linalokukwamisha wewe kupata kile unachotaka?
Imani yoyote ile inayokuzuia wewe usipige hatua siyo imani nzuri kwako.
Kitu kimoja cha mwisho, kuwa na imani ambazo zitakufikisha kule unakotaka kufika. Je, imani ulizonazo kwenye eneo la fedha unafikiri zitakufikisha kweli kule unakotaka kufika?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog