Kitu hicho ni uaminifu.
Uaminifu ni msingi muhimu sana.
Yote tuliyojifunza hapa na tunayoendelea kujifunza hapa hayatawezekana kama utakosa kitu kimoja ambacho ni uaminifu.
Unahitaji kuwa na uaminifu wa hali ya juu sana.
Wakati mwingine uaminifu wako utakukosesha wateja, hasa pale utakapowaeleza ukweli kwamba kile wanachohitaji hasa wewe huna.
Ni bora useme ukweli kuliko kudanganya, kama kitu huna sema na usidanganye.
Kwa mfano, unaweza ukawadanganya wateja wako kwamba una kile ambacho wao wanachotaka na ukawapatia lakini kinakuja kisiwafae, watakosa imani na wewe na watawaambia watu wengine na hapo utakua umejiharibia mwenyewe.
Hatua ya kuchukua leo; Kuwa mwaminifu na timiza kile unachoahidi na hakikisha unampa mtu au mteja wako kile hasa anachotaka na kitakachokwenda kumsaidia.
Kitu kimoja cha mwisho, uaminifu ni msingi muhimu sana, usitegemee kuupata kwa watu wa kawaida.
Chochote unachokifanya kifanye kwa uaminifu na utaona matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye kile unachofanya.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog