Hakuna Mtazamo Wa Hovyo Duniani Kama Huu

Kwenye kitabu chake jinsi ya kuuza chochote mwandishi Joe Girard anatuambia hakuna mtazamo wa hovyo duniani kama kuamini kwamba kitu hakiwezi kufanyika kwa sababu hakijawahi kufanywa. Mtazamo huo ndiyo umewafanya wengi kushindwa kupiga hatua, kwa kuendelea na mazoea. Hata kama hakuna mtu mwingine amewahi kufanya kitu fulani, kama umeona ndiyo unapaswa kukifanya ili kupata matokeo …

Asante Ya Mtu Huyu Inapaa Mbinguni

Huwa tunafikiri kutafuta ufalme wa Mungu ni kusali na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada mara nyingi. Sina uhakika kama itakufaa lakini kutafuta ufalme wa Mungu ni pamoja na kusaidia watu wake. Hata yule anayesali sana hajawahi kumuona Mungu kwa macho, ni katika kusaidia watu wake ndiyo tunamuona Mungu kwa macho. Unaposaidia watu kupitia kile unachofanya, …

Jilazimishe Kuishiwa Kiakili Kwenye Eneo La Fedha

Kutoka kwenye kitabu cha Tano za Majuma Ya Mwaka, kilichoandikwa na Kocha Dr Makirita Amani, kuna dhana ambayo nilijifunza katika eneo la fedha, nimeona ni vema na wewe nikushirikishe. Karibu sana rafiki yangu, "Kilio cha wengi kwenye fedha ni kwamba, watu wakipata fedha haikai na hata wakiweka akiba, haikai. Yaani wakipata fedha au wakiwa na …

Ukitaka Kuharibu Mahusiano Yako Kuwa Mtu Wa Hivi

Kuna baadhi ya changamoto kwenye mahusiano huwa tunazinunua sisi wenyewe kwa kujitakia. Sisi binadamu ni viumbe vya hisia, hivyo unapokuwa katika mahusiano na watu wengine jitahidi sana kuangalia hisia za watu. Watu wanafanya maamuzi yao kwa hisia, na siyo kwa fikra. Ukitaka kuharibu mahusiano yako na watu wengine kuwa mkosoaji. Hakuna mtu anayependa kukosolewa. Ukitaka …

Jinsi Ya Kujua Kama Unaenda Mbele Au Unarudi Nyuma Kiuchumi

Siku moja nilikuwa nasafiri kuelekea Dodoma kwenye semina, nikakutana na rafiki kwenye gari. Alinieleza ni kwa jinsi gani amekuwa hana nidhamu ya fedha, hajui afya ya kipato chake. Siyo yeye tu, wako wengi ambao hawajijui kama wanaenda mbele kiuchumi au wanarudi nyuma kiuchumi. Nilimuuliza rafiki niliyekutana naye kwenye gari, je, unaweza kuniambia matumizi yako ya …

Hasara Moja Ya Kuwa Mvivu

Hakuna dhambi ambayo inawafanya watu wengi kutokufanikiwa kwenye maisha yao kama uvivu. Uvivu ndiyo chanzo cha watu wengi kutokupiga hatua. Sina uhakika kama itakufaa lakini unapokuwa mvivu unakuwa unawavunjia heshima wale wote wanaokuamini. Ikiwa utakua mvivu basi nakuhakikishia utakuwa unawavunjia heshima wale wote ambao wanaokuamini na hiyo ndiyo hasara moja ya uvivu. Pata picha ni …

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Wateja Wakae Na Wewe Kwa Muda Mrefu

Kila biashara inahitaji mteja ili iweze kuendelea, maisha ya biashara yanategemea mteja kwa sababu mteja ndiyo analeta fedha. Mteja ndiyo anafanya mauzo yaweze kwenda vizuri kwenye biashara yako, mauzo ndiyo moyo wa biashara. Na biashara nyingi zenye changamoto ukichunguza vizuri shida inaanzia kwenye mauzo. Mauzo yakishakuwa chini utashindwa kujiendesha kibiashara na hatimaye utashindwa kulipa bili …

Kiwango Cha Fedha Kinachowatesa Watu Wengi

Kadiri ya Grant Cardone kuna aina tatu za fedha lakini mimi leo niko hapa kukuambia kiwango kinachowatesa watu wengi na kushindwa kusonga mbele kwenye eneo la fedha. Aina ya kwanza ya kiwango hiko cha fedha kinachowatesa watu ni kiwango cha hofu. Kiwango cha hofu katika fedha kikoje kwani? Kiwango cha hofu hiki ni kiwango cha …

Usikadirie Chochote Kile

Usikadirie chochote kile, wewe weka juhudi kadiri uwezavyo lakini usilazimishe matokeo unayotaka wewe. Matokeo yako nje ya uwezo wako, lakini mchakato wa kitu chochote kile uko ndani ya uwezo wako. Usifanye kitu halafu ukakadiria matokeo maana matokeo yanaweza kukuumiza vibaya na ukachukia hata kuendelea na mchakato. Wewe weka juhudi kadiri unavyoweza lakini usilazimishe matokeo yawe …

Jinsi Ya Kuendelea Kuvuna Kwa Mteja Wako

Wale watu ambao wanategemea kupata huduma yako kupitia kazi au biashara yako ndiyo wateja wako. Hata kama wewe ni mzazi basi watoto ni wateja wako, unatakiwa kuwapa huduma bora ya malezi kuwahi kutokea duniani. Wewe kama ni mke au mume unatakiwa kutoa huduma bora kwa mteja wako ambaye ni mke au mume wako. Wewe kama …

Design a site like this with WordPress.com
Get started