Wale watu ambao wanategemea kupata huduma yako kupitia kazi au biashara yako ndiyo wateja wako.
Hata kama wewe ni mzazi basi watoto ni wateja wako, unatakiwa kuwapa huduma bora ya malezi kuwahi kutokea duniani.
Wewe kama ni mke au mume unatakiwa kutoa huduma bora kwa mteja wako ambaye ni mke au mume wako.
Wewe kama kiongozi wa imani shehe, Padre au mchungaji waumini wako ndiyo wateja wako unapaswa kuwahudumia vizuri.
Na tunapaswa kufanya hivyo kwa uaminifu mkubwa mno ili uendelee kuvuna kwa muda mrefu.
Ukishakuwa ni mtu mdanganyifu, utapoteza wateja kwa sababu wateja wakishajua unawadanganya hawataendelea kufanya kazi na wewe.
Ila ukiwa mwaminifu kwenye kile unachofanya nakuhakikishia utaendelea kuvuna matokeo mazuri.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa mwaminifu kwenye kile unachofanya na utaendelea kuvuna matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.
Baki kwenye mchakato wa uaminifu kuna manufaa makubwa kuliko kuhangaika na vitu visivyokuwa na uaminifu.
Chochote kile unachokifanya kwa upendo, na anayepokea huduma yako akafurahia hiyo ni sala inayopaa mbinguni.
Tunapoambiwa tafuteni kwanza ufalme wa Mungu, maana yake ni kusaidia watu wake kwanza unapomsaidia mtu na ajafanikiwa unakuwa umeutafuta ufalme wa Mungu. Watumikie watu wake Mungu ndiyo namna bora ya kutafuta ufalme wa Mungu.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog