Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Wateja Wakae Na Wewe Kwa Muda Mrefu

Kila biashara inahitaji mteja ili iweze kuendelea, maisha ya biashara yanategemea mteja kwa sababu mteja ndiyo analeta fedha.

Mteja ndiyo anafanya mauzo yaweze kwenda vizuri kwenye biashara yako, mauzo ndiyo moyo wa biashara. Na biashara nyingi zenye changamoto ukichunguza vizuri shida inaanzia kwenye mauzo.

Mauzo yakishakuwa chini utashindwa kujiendesha kibiashara na hatimaye utashindwa kulipa bili mbalimbali kama vile kujilipa wewe mwenyewe, kuwalipa wengine nk.

Biashara ikiwa haina mauzo maana yake haina fedha. Na fedha ndiyo damu yenyewe, pata picha mwili wa binadamu ukikosa damu nini kinatokea?

Kiasili maisha ya binadamu ni biashara, uwe umejiajiri au umeajiriwa.

Unaweza ukazitumia mbinu hizi ambazo nakushirikisha siyo tu kwenye kazi, biashara lakini pia hata katika mahusiano mengine.

Rafiki yangu nikupendaye, mteja wako anapokaa na wewe muda mrefu ndivyo unavyonufaika zaidi.

Hivyo basi, unahitaji kuweka juhudi kuhakikisha wateja wako wanabaki na wewe kwa muda mrefu.

Zifuatazo ni njia za kuongeza thamani ya maisha ya wateja wako kwenye biashara yako.

Moja. Toa huduma bora sana kwa wateja wako ambazo hawawezi kuzipata sehemu nyingine yoyote ile isipokuwa kwako tu.

  1. Kutengeneza mahusiano mazuri na wateja wako. Wafanye wateja wako kuwa rafiki kwajo6na kwenye biashara yako pia.
    Wajione siyo tu wanakuja kununua, bali wanakuja kwa rafiki yao anayewajali na kuwapa kile kilicho sahihi kwao.
  2. Weka mbele maslahi ya wateja wako na siyo faida unayotaka kupata tu, usiwe mtu wa kutaka kuwapiga tu wateja, jali maslahi ya wengine na yako yatakuja yenyewe.
  3. Waelimishe wateja wako, washauri vizuri hata kama utapoteza mauzo lakini hilo litawajengea imani zaidi na hivyo kuendelea kukuamini na kununua zaidi.
  4. Wafanye wateja wako kuwa mashabiki wa biashara yako. Ukiwafanya wateja wako kuwa mashabiki zako wa kweli, wataweza kuitangaza biashara na kuwa sehemu ya biashara yako na kukutangazia kwa wengine.

Hatua ya kuchukua leo; tumia njia hizi tano za kuongeza thamani ya maisha kwa wateja wako.

Ukitumia mbinu hizi, zitakusaidia kuongeza wateja wapya na wateja tarajiwa. Kikubwa toa thamani kubwa kwa wengine na mambo mazuri yatakuja yenyewe.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: