Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kujua Kama Unaenda Mbele Au Unarudi Nyuma Kiuchumi

Siku moja nilikuwa nasafiri kuelekea Dodoma kwenye semina, nikakutana na rafiki kwenye gari. Alinieleza ni kwa jinsi gani amekuwa hana nidhamu ya fedha, hajui afya ya kipato chake.

Siyo yeye tu, wako wengi ambao hawajijui kama wanaenda mbele kiuchumi au wanarudi nyuma kiuchumi.

Nilimuuliza rafiki niliyekutana naye kwenye gari, je, unaweza kuniambia matumizi yako ya fedha kwa mwezi uliopita yalikuwa kiasi gani?
Alijibu, hapana hajui hata huwa anatumia shilingi ngapi kwa mwezi.
Mimi nilimjibu hata ukiniuliza kipato changu ya mwezi wowote hata mwaka jana najua kwa sababu ninayo rekodi na angalia tu, alishangaa sana na akaahidi kuwa pamoja na mimi ili niwe namfundisha kwenye nidhamu ya fedha.

Je, wewe unajua matumizi yako ya mwezi julai yalikuwa kiasi gani?

Ili uweze kujua jumla ya kipato chako kwa mwezi julai na matumizi yako unapaswa kufanya tathimini.

Na ni ngumu kufanya tathmini kama huna data yaani taarifa. Utajuaje sasa mwezi julai umetumia kiasi gani kama ulikuwa huandiki rekodi?
Unapaswa kuwa na daftari la kuandika kumbukumbu za matumizi yako ya kila siku na kipato unachoingiza kila siku.

Ili inapofika mwisho wa mwezi unajua jumla ya kipato chako ni kiasi na matumizi yako ni kiasi gani.

Kama matumizi yako yanazidi kipato chako basi hali yako ya kiuchumi ni mbaya. Matumizi yako yanatakiwa yasizidi kipato.

Haijalishi unapata kipato kikubwa kiasi gani, unapaswa kuishi chini ya kipato chako ( whatever your income, live below your means)

Kama kipato chako ni kikubwa kuliko matumizi, basi hali yako ya kiuchumi ni nzuri sana.

Kwa mfano, kipato chako kwa mwezi ni laki tano na matumizi yako ya kifedha ni laki 6 na elfu 10 hapo hali yako ya kifedha ni mbaya kwa sababu hiyo hela iliyoongezeka hapo utakua umeikopa kufanya matumizi na kitu ambacho siyo sahihi kufanya.

Kama kipato chako ni laki tano halafu matumizi yako ni laki 4 basi hali yako ya kifedha ni nzuri.

Bado watu wengi wanaishi kimazoea huku wakiwa hawana elimu ya msingi ya fedha, na ubaya ni kwamba hawajui kama hawajui na hawataki kujifunza.

Hatua ya kuchukua leo; leo nunua daftari la mapato na matumizi na anza kuandika kila fedha inayoingia na inayotoka bila kuacha kwa mwezi mzima na mwisho wa mwezi tarehe kama ya leo utakua na kitu cha kuripoti.

Ijue afya yako kifedha, wakati mwingine unaweza ukajiona unaenda mbele kumbe unarudi nyuma kwa njia ya kukaa chini na kufanya tathmini utapata ukweli wa maisha yako.

Na habari njema ni kwamba, mimi rafiki yako ninayo maswali ya muongozo wa wewe kujifanyia tathmini ya mwezi julai, unachotakiwa kufanya ni wewe kujiunga na Mimi Ni Mshindi Klabu ili uweze kupata mafunzo mbalimbali.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: