Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kiwango Cha Fedha Kinachowatesa Watu Wengi

Kadiri ya Grant Cardone kuna aina tatu za fedha lakini mimi leo niko hapa kukuambia kiwango kinachowatesa watu wengi na kushindwa kusonga mbele kwenye eneo la fedha.

Aina ya kwanza ya kiwango hiko cha fedha kinachowatesa watu ni kiwango cha hofu.

Kiwango cha hofu katika fedha kikoje kwani?

Kiwango cha hofu hiki ni kiwango cha fedha ambacho unakuwa nacho lakini kinakupa hofu zaidi.

Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na akiba kidogo lakini anaogopa kukitumia sababu anawaza ikitokea akiba aliyokuwa nayo imepotea je, atawezaje kupata fedha zaidi?

Hiki ni kiwango cha fedha ambacho ni kifungo na utumwa wa fedha. Ni kiwango cha kimsikini na unapaswa ukiepuke kabisa.

Kiwango hiki kinakuzuia kupata fedha zaidi. Unaogopa kuzalisha fedha zaidi kwa sababu ya kuogopa kutumia fedha uliyokuwa nayo kwa ajili ya kupata fedha zaidi.

Hatua ya kuchukua leo; unapaswa kuwa na kiwango cha fedha ambacho unakuwa tayari kukitumia kwa ukuaji zaidi.

Kitu kimoja cha mwisho, ukiwa na kiwango cha ukuaji kitakusaidia kuwekeza kwako binafsi na kuwekeza kwenye biashara zako kitu ambacho kitakusaidia kukuza kipato chako zaidi.

Kadiri unavyowekeza kwako binafsi na kwenye biashara, kukua zaidi kwenye fedha utashangaa kipato chako pia kinaongezeka.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: