Ukitaka kuiona hela ongeza kipato na punguza matumizi yasiyokuwa na ulazima kwenye maisha yako. Ni kweli utapunguza sana matumizi lakini kuna matumizi mengine hata upunguze vipi bado ni muhimu sana. Ili maisha yako yaende lazima ufanye matumizi hayo. Yako matumizi yasiyokuwa na ulazima na yako ambayo yanaulazima, huwezi kuyaacha kwa sababu bila hayo maisha yako …
Haya Ndiyo Maisha Ya Furaha
Watu wengi huwa wanapenda kujiingiza katika maisha ya msongo kwa kununua matatizo ya kujitakia. Huwa tunahangaika na mambo mengi ambayo yako nje ya uwezo wetu ndiyo maana tunakosa furaha. Tukishindwa kuyadhibiti basi tunakuwa na maisha ya msongo. Mwanafalsafa wa ustoa, Epictetus anasema maisha ya furaha ni pale unapojua kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako …
Miaka 6 Ya Kuandika Kila Siku Na Mambo Kumi Ya Kujifunza
Ilikuwa ni tarehe moja mwezi octoba mwaka 2016 ndipo nilianza marathoni ya kuandika kila siku bila kuacha. Namshukuru Mungu kwa yote katika kipindi chote cha miaka 6 ya kuandika kila siku. Yako mengi ambayo unaweza kujifunza kupitia kazi yangu ya uandishi. Kuandika ni kazi kama zilivyo kazi nyingine lakini ni kazi ngumu kwa sababu inahitaji …
Continue reading "Miaka 6 Ya Kuandika Kila Siku Na Mambo Kumi Ya Kujifunza"
Kama Umepanda Gari Sahihi
Unapata wasiwasi gani wa safari? Kwa mfano, umepanda gari lako la kwenda Arusha, lakini ukiwa kwenye gari unaanza kujiuliza sasa mbona Arusha hatufiki? Kama umepanda gari sahihi usiwe na wasiwasi utafika kule unakokwenda. Hii ina maana kwamba, ukikaa kwenye mchakato sahihi wa kufanya kitu fulani usiwe na wasiwasi na matokeo. Kwa sababu matokeo mazuri yatakuja …
Tunza Uadilifu wako
Uadilifu ni kuishi kile ulichoahidi na unachosimamia kwa mfano, umeahidi utakua mwaminifu katika maisha yako. Basi unaishi kile ambacho umekiahidi na ukienda kinyume maana yake umevunja uadilifu wako. Uadilifu wako una thamani kubwa kuliko almasi hivyo basi, usifanye chochote kile cha kuharibu uadilifu wako kwa sababu ukishauchafua ni vigumu kuusafisha. Umekula kiapo cha kuwa mwaminifu …
Ulishawahi Kukutana Na Hali Hii Ukipata Fedha?
Iko wazi kwamba, kuna watu ambao wakipata fedha zinakuwa zinawawasha yaani wanakuwa hawawezi kutulia nazo mpaka ziishe. Kwa sababu watu wengi wanakutana na hali hii, leo nataka kukusaidia kupata suluhisho lake. Kama unapata fedha na huwezi kutulia nazo ni rahisi watu kukujua na kukulaghai wanapojua una fedha. Suluhisho la hili rafiki yangu nikupendaye, unapaswa kujijengea …
Continue reading "Ulishawahi Kukutana Na Hali Hii Ukipata Fedha?"
Njia Rahisi Ya Kuwapoteza Wateja Wako
Uwe unafanya biashara au hufanyi lakini kiasili kila mtu ana mteja wake kwa sababu kuu moja ambayo ni kila mtu ni muuzaji. Kwa sababu kama huna unachouza utayaendeshaji maisha yako? Wako wanaouza huduma, ujuzi, maarifa, uzoefu, muda nk. Kitu muhimu sana wewe kama muuzaji unachotakiwa kufanya ni kutimiza ahadi unazotoa. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanawadanganya wateja …
Hii Ndiyo Maana Ya Mafanikio
Watu wengi hawana uelewa juu ya mafanikio. Hata wale ambao tunawaona wamefanikiwa kwa nje ni wachache sana ambao wamefanikiwa. Wengi wanapima mafanikio kwa vitu ambavyo mtu anavyo kama vile gari au nyumba. Kifupi tu, kuwa na nyumba au gari siyo mafanikio bali kitu cha kawaida kwa binadamu kuwa nacho. Kwa mfano, wewe unakula kila siku, …
Tabia Inayowashinda Watu Wengi
Ni uaminifu. Watu wameshindwa kuwa waaminifu kwao wenyewe na kwa wengine. Uaminifu ndiyo mtaji unaolipa kwenye kila eneo la maisha yetu. Kuanzia kazi, mahusiano, biashara na nk. Kama kila mmoja angekuwa mwaminifu tu kwenye mambo madogo ambayo anajiwekea kufanya na angeyafanya basi dunia ingekuwa sehemu salama sana. Usiishi kwa kufuata mkumbo wa watu, kama watu …
Hiki Ndicho Unachopaswa Kukilinda Kuliko Vitu Vingine Vyote
Mpaka hapo ulipo tayari kuna sifa ambazo umeshajijengea na unajivunia kuwa nazo kwako wewe mwenyewe na kwa watu wengine. Umetumia muda mrefu kujenga sifa na jina lako. Hivyo basi, unapaswa kulinda sifa ulizojijengea pia ili juhudi zako zisipotee bure. Usikubali kufanya jambo ambalo litakuja kuharibu sifa yako hata siku moja. Shabaha yangu kubwa leo ni …
Continue reading "Hiki Ndicho Unachopaswa Kukilinda Kuliko Vitu Vingine Vyote"