Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ulishawahi Kukutana Na Hali Hii Ukipata Fedha?

Iko wazi kwamba, kuna watu ambao wakipata fedha zinakuwa zinawawasha yaani wanakuwa hawawezi kutulia nazo mpaka ziishe.

Kwa sababu watu wengi wanakutana na hali hii, leo nataka kukusaidia kupata suluhisho lake.

Kama unapata fedha na huwezi kutulia nazo ni rahisi watu kukujua na kukulaghai wanapojua una fedha.

Suluhisho la hili rafiki yangu nikupendaye, unapaswa kujijengea tabia za fedha ambazo hazikufanyi uonekane kwa kila mtu wakati ambapo una fedha na ambapo huna fedha.

Ukifanikiwa kujijengea tabia hiyo, utajiepusha na matatizo mengi kwenye maisha yako.

Maana fedha zikiwepo huwa hazikosi matumizi yasiyokuwa na ulazima.

Hatua ya kuchukua leo; unapopata fedha zaidi ya ulivyozoea kupata, jifunze kutulia kwanza kabla hujafanya maamuzi au chochote kile.

Jifunze kuchukulia kama vile hujapata fedha hizo. Kuwa kama vile huna kitu, endelea kuyaendesha maisha yako kama yalivyokuwa kawaida.

Maana watu wakipata fedha akili huwa zinahama hivyo ukishakuwa umetulia ndiyo unaweza kupanga kipi cha kufanya na fedha zako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: