Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tunza Uadilifu wako

Uadilifu ni kuishi kile ulichoahidi na unachosimamia kwa mfano, umeahidi utakua mwaminifu katika maisha yako. Basi unaishi kile ambacho umekiahidi na ukienda kinyume maana yake umevunja uadilifu wako.

Uadilifu wako una thamani kubwa kuliko almasi hivyo basi, usifanye chochote kile cha kuharibu uadilifu wako kwa sababu ukishauchafua ni vigumu kuusafisha.

Umekula kiapo cha kuwa mwaminifu katika maisha yako ya ndoa na ukiishi kinyume chake maana yake umekosa uadilifu.

Umekula kiapo cha kuwa kiongozi mwaminifu lakini unachofanya ni kinyume na uadilifu hapo unakuwa unaishi kinyume na misingi ya uadilifu.

Viko vitu vingi ambavyo umeahidi, unapaswa kuwa mwadilifu hadharani na faraghani. Usiwe mwaminifu hadharani tu, bali sehemu zote.

Watu wakishajua kwamba wewe siyo mwadilifu, hawakuthamini tena. Na hakuna hukumu mbaya kama hukumu ya umma.

Hatua ya kuchukua leo; fanya mambo yako kwa uaminifu na uadilifu na simamia hilo kama sheria kwako iwe hadharani au faraghani.

Ikitokea utakosa fedha kwa sababu ya kusimamia uadilifu, kubali tu kukosa fedha hizo kwa sababu haya ukizipata kuna wakati utapaswa kuzirudisha na itaacha madhara makubwa sana kwako kwa sababu watu hawatakuamini tena.

Jamii ikishakosa uaminifu na uadilifu kutoka kwako, ni ngumu sana kukupa mrejesho chanya. Ukikosa kuaminika na jamii maana yake umepoteza mauzo na mauzo ndiyo yanayoleta fedha na sidhani kama watu watapenda kununua kwa mtu ambaye ameshapoteza sifa ya uadilifu na uaminifu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: