Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Maisha Ya Furaha

Watu wengi huwa wanapenda kujiingiza katika maisha ya msongo kwa kununua matatizo ya kujitakia.

Huwa tunahangaika na mambo mengi ambayo yako nje ya uwezo wetu ndiyo maana tunakosa furaha. Tukishindwa kuyadhibiti basi tunakuwa na maisha ya msongo.

Mwanafalsafa wa ustoa, Epictetus anasema maisha ya furaha ni pale unapojua kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako na kile ambacho kipo nje ya uwezo wako.

Ukifuata kauli hiyo hutapata msongo kabisa kwa sababu unajua kuna vitu viko ndani ya uwezo wako na vingine viko nje ya uwezo wako hivyo hauna udhibiti navyo.

Hatua ya kuchukua leo; Kama umekutana na jambo kitu cha kwanza jiulize, je kipo ndani ya uwezo wangu? Au kipo nje ya uwezo wangu?
Kikiwa ndani ya uwezo wako chukua hatua na kikiwa nje ya uwezo wako achia asili au wenye mamlaka wapambane nacho kwa mfano, kukatika kwa umeme au mvua kutokunyesha ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako.

Kama kitu kipo nje ya uwezo wako usijilazimishe kuingia kwenye mtego wa msongo, achana nacho au angalia namna unavyoweza kukikabili kama kilivyo na kuendelea na mengine na badala ya kuhangaika na msongo ambao hautakusaidia.

Kuwa na furaha au kutokuwa na furaha ni kujitakia kwa sababu watu wanakosa furaha pale mambo yanapoenda tofauti na walivyopanga na mambo yanaenda vizuri ni pale mambo yanapoenda kama walivyopanga.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: