Design a site like this with WordPress.com
Get started

Utabana Matumizi Mpaka Lini?

Ukitaka kuiona hela ongeza kipato na punguza matumizi yasiyokuwa na ulazima kwenye maisha yako.

Ni kweli utapunguza sana matumizi lakini kuna matumizi mengine hata upunguze vipi bado ni muhimu sana.

Ili maisha yako yaende lazima ufanye matumizi hayo.

Yako matumizi yasiyokuwa na ulazima na yako ambayo yanaulazima, huwezi kuyaacha kwa sababu bila hayo maisha yako hayawezi kwenda.

Utabana matumizi mpaka lini na vitu ambavyo unataka kufanya ni muhimu?

Liko suluhisho ambalo ni kuongeza kipato zaidi.

Gharama za maisha zimepanda, vitu vingi vimepanda bei hata ukilalamika haitokusaidia kupunguza gharama.

Maisha yanapaswa yaendelee. Ili uweze kukabiliana na gharama za maisha unapaswa tu kujitoa kafara katika kuongeza kipato zaidi ili upate fedha za kulipa bili mbalimbali ambazo zinajitokeza kwenye maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo; kama unapenda kuishi maisha mazuri na usikose fedha za kulipia bili mbalimbali unazopaswa kulipa ongeza kipato zaidi.

Kama matumizi umeshapunguza sana na ujanja sasa ni kuongeza kipato chako ili uweze kukabiliana na gharama za maisha zinazopanda kila siku.

Kama maisha yanapanda na wewe panda kwa kuongeza kipato zaidi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: