Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndicho Unachopaswa Kukilinda Kuliko Vitu Vingine Vyote

Mpaka hapo ulipo tayari kuna sifa ambazo umeshajijengea na unajivunia kuwa nazo kwako wewe mwenyewe na kwa watu wengine.

Umetumia muda mrefu kujenga sifa na jina lako. Hivyo basi, unapaswa kulinda sifa ulizojijengea pia ili juhudi zako zisipotee bure.

Usikubali kufanya jambo ambalo litakuja kuharibu sifa yako hata siku moja.

Shabaha yangu kubwa leo ni kutaka kukuambia kuwa, sifa ndiyo kitu pekee unachopaswa kukilinda kuliko vitu vingine vyote.

Ukipoteza sifa yako unakuwa umepoteza maisha yako. Watu ambao walikuwa wanakuamini na kukutegemea utakua umewapoteza kwa mfano, kama ni kwenye biashara ulijenga sifa ya uamini na siku moja tu ukafanya vitu ambavyo siyo vya uaminifu unakuwa umepoteza sifa yako.

Hatua ya kuchukua leo; Linda sifa yako uliyojijengea au unayoendelea kujijengea kwa gharama yoyote ile.

Usikubali kamwe kuharibu sifa uliyojijengea kwa mtu ambaye anakuamini kwa sifa ambayo tayari umeshajijengea kwake.

Kitu cha mwisho cha kuondoka nacho hapa ni linda sifa yako kuliko vitu vingine vyote kwa sababu hakuna kitu ambacho kinalipa kama sifa ambayo tayari umejijengea na watu wanaiamini kutoka kwako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: