Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tabia Inayowashinda Watu Wengi

Ni uaminifu.

Watu wameshindwa kuwa waaminifu kwao wenyewe na kwa wengine.

Uaminifu ndiyo mtaji unaolipa kwenye kila eneo la maisha yetu. Kuanzia kazi, mahusiano, biashara na nk.

Kama kila mmoja angekuwa mwaminifu tu kwenye mambo madogo ambayo anajiwekea kufanya na angeyafanya basi dunia ingekuwa sehemu salama sana.

Usiishi kwa kufuata mkumbo wa watu, kama watu wengine siyo waaminifu haimaanishi kwamba na wewe usiwe mwaminifu.

Dunia ya leo ina changamoto kubwa sana ya watu sahihi, mpaka inaamua kuzalisha maroboti kwa ajili ya kufanya kazi ambazo zilitakiwa kufanywa na watu.

Lakini bado watu ni wa muhimu hata uwe na maroboti.

Watu wanalalamika kazi hakuna, hakuna mitaji ya kuanzisha biashara, hakuna watu sahihi. Lakini, je, swali la kujiuliza utawezaje kupata mtu sahihi kama wewe siyo mtu sahihi?

Duniani hakuna changamoto ya kazi, bali kuna changamoto ya watu sahihi wa kufanya kazi.

Mtu anayekuambia sijapata ajira jua ana tabia fulani iliyomfanya asipate ajira.

Mtu akikuambia sina biashara jua kuna tabia ambayo inamkwamisha asiwe na biashara.

Kama una thamani utakosaje kazi ya kufanya?

Ukiwa mwaminifu kwako wewe mwenyewe huwezi kukosa kile unachotaka kwenye maisha yako.

Uaminifu ni kama ukweli huwa unajitetea wenyewe.

Sina uhakika kama itakufaa lakini nakusihi sana kuwa mwaminifu kwenye maisha yako na utaishi kwa amani na utapata matokeo mazuri zaidi.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa mwaminifu kwako wewe mwenyewe na kwa wengine.

Ukiweza kujijengea tabia ya uaminifu, mafanikio makubwa kwako ni suala la muda.

Wafundishe watu uaminifu kupitia wewe mwenyewe. Maisha yako yakiwa hayana kona kona yanawabariki wengine hata unakuwa na amani kuyaelezea.

Mtu ambaye hana uaminifu kwenye maisha yake, anakuwa na wasiwasi kama vile anaoga nje.

Kwanini ujitese ndugu, kifupi kuwa mwaminifu kwenye kila eneo la maisha yako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: