Design a site like this with WordPress.com
Get started

Miaka 6 Ya Kuandika Kila Siku Na Mambo Kumi Ya Kujifunza

Ilikuwa ni tarehe moja mwezi octoba mwaka 2016 ndipo nilianza marathoni ya kuandika kila siku bila kuacha.

Namshukuru Mungu kwa yote katika kipindi chote cha miaka 6 ya kuandika kila siku.

Yako mengi ambayo unaweza kujifunza kupitia kazi yangu ya uandishi. Kuandika ni kazi kama zilivyo kazi nyingine lakini ni kazi ngumu kwa sababu inahitaji utulivu wa akili, uwe umefanya uwekezaji wa maarifa na uweze kutoa.

Huwezi kutoa kile ambacho huna, hivyo basi kuandika kwangu imekuwa ni kama sala pale tu ninapopata bahati ya kuiona siku inakuwa ni siku ya utoaji kwangu.

Napenda sana kutoa na nina amini katika kutoa ndiyo tunapokea. Na pale ninapotoa ndiyo napata ridhiko la ndani.

Katika miaka hii sita ya uandishi nimejifunza yafuatayo;

Moja kila kitu kinawezekana. Kuwa na ndoto kubwa na kisha anzia pale ulipo.

Mbili, nidhamu binafsi.
Kama unataka kufanikiwa kwenye maisha yako kuwa na nidhamu binafsi, jitume sana na jisimamie mpaka upate kile unachotaka bila kuishi njiani.

  1. Usitafute sababu, tafuta matokeo. Katika kipindi hiki cha miaka 6 ya kuandika kila siku sijawahi kutoa sababu yoyote ile kwa wasomaji wangu kwamba leo ninaumwa au sijikii vizuri. Kwa yeyote anayenifuatilia kila siku akiamka lazima atapata makala bila kujali sababu yoyote ile.
    Watu wanajali matokeo na siyo sababu zako za kushindwa kwa sababu kila mtu anaweza kutoa sababu hivyo jitofautishe kwa kuleta matokeo mazuri.
  2. Anika ndoto yako kubwa. Iambie dunia kabisa kwamba ndoto yako kubwa ni nini na kisha ifanyie kazi. Kwa mfano mimi nilivyoanza nilianika ndoto yangu ya kuandika kila siku ya maisha yangu mpaka siku yangu ya mwisho kuvuta pumzi.
    Hii inanisukuma kwamba napaswa kuandika na dunia nimeshaiambia nisipofanya hivyo nitakuwa naidanganya.
  3. Hakuna mafanikio makubwa bila maumivu. Wakati naanza kuandika kila siku ilikuwa changamoto, lakini nilivumilia maumivu na kujenga tabia ya kuandika kwa sasa kuandika imekuwa kama kupumua kwani huwezi kuishi bila kupumua.

Sita, usikubali kuvunja mnyororo, usikubali kuishi njiani ukianza kitu kuwa king’ang’anizi mpaka upate matokeo.

Saba, wale ambao wanakuambia haiwezekani, wadhihirishie kwamba inawezekana kabisa kwa kufanya kwa vitendo. Mwanzoni nilipata upinzani kwamba sitofika mbali lakini nilikataa hilo na kuwaambia kila kitu kinawezekana.

Nane, usipokuwa na maarifa sahihi na kitu unachosimamia ni rahisi kuyumbishwa. Soma sana vitabu, jifunze kwa watu waliofanikiwa kwenye eneo unalotaka kukua. Usiposimama kwa kitu utaanguka kwa chochote kile.

Tisa, waepuke watu hasi kabisa kwenye maisha yako. Ukikaa na mtu aliyejipaka kinyesi na wewe utanuka kinyesi. Watu hasi ni hatari na ndiyo wanaofanya dunia isiende mbele. Zungukwa na watu chanya ambao wanakupa maarifa mapya kila siku.

Kumi, kuwa bora kiasi kwamba hakuna atakayeweza kukupuuza kwenye maisha yako. Watu wanakuchulia vile unavyojichukulia wewe. Jichukulie wewe ni mtu wa thamani, kwa kufanya mambo yako kwa viwango vya juu ambavyo hata wao hawawezi kuvifikia.

Hatua ya kuchukua leo; Sina uhakika kama itakufaa lakini kuwa na kitu kimoja ambacho utakua unakifanya kila siku. Hata siku mambo yakienda vibaya unashukuru kwamba licha ya mambo kwenda vibaya nashukuru leo nilifanikiwa kufanya kitu fulani.
Kwa mfano, ushindi wangu wa kwanza kabla sijatoka nyumbani kwenda kuwatumikia wengine ni kuandika.

Hakikisha kabla hujatoka nyumbani, basi umefanya kitu ambacho kimekuja ushindi, usitoke tu kitandani kwa kuchelewa kuwahi kuvaa na kwenda kazini. Amka mapema asubuhi, weka orodha ya vitu vya kufanya yaani to Do List jifunze, sali, andika, soma malengo yako jinenee maneno chanya. Toka kwenye mlango wa chumba chako ukiwa na furaha na jiambie leo ni siku bora sana kwangu kufanya makubwa na nimechagua leo kuwa siku ya furaha kwangu sitoruhusu chochote kile kiharibu utulivu wangu wa akili.

Mwisho, ukifanya mambo makubwa, ukienda hatua za juu kuliko watu wengine watu wanaanza kukuogopa na wanaacha kabisa kukuwekea upinzani. Tafuta kitu kimoja ambacho utaapa kukifanya mpaka kufa kwako, hata siku ukifa dunia itajivunia kupitia kile ulichofanya. Kwa chochote unachotaka usichukulie wengine watasemaje ila jiangalie wewe mwenyewe kwanza.
Sikiliza moyo wako unataka nini na kisha fuata moyo wako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: