Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Maana Ya Mafanikio

Watu wengi hawana uelewa juu ya mafanikio. Hata wale ambao tunawaona wamefanikiwa kwa nje ni wachache sana ambao wamefanikiwa.

Wengi wanapima mafanikio kwa vitu ambavyo mtu anavyo kama vile gari au nyumba.

Kifupi tu, kuwa na nyumba au gari siyo mafanikio bali kitu cha kawaida kwa binadamu kuwa nacho. Kwa mfano, wewe unakula kila siku, unaweza ukasimama mbele ya watu na kujisifu kuwa umekula?

Au unaoga kila siku, au umenunua nguo unaweza ukasimama mbele ya watu na kujivunia kuwa umenunua nguo?

Kumbe basi hivyo ni vitu vya kawaida kabisa, kwa mtu yoyote anapaswa kuwa navyo kwa sababu ni mahitaji ya msingi ya binadamu anayopaswa kuwa nayo.

Kuwa na nyumba au gari ni mafanikio ambayo hayagusi watu wengine. Lakini, muuza chips mtaani kwako huenda akawa anagusa maisha ya watu wengine kuliko wewe ambaye una miliki vitu ambavyo havigusi maisha ya wengine bali ni wewe tu na familia yako.

Kwahiyo, maana ya mafanikio kwenye jamii yetu ni ndogo sana na watu wanacheza ligi ndogo za mchangani na siyo ligi kuu.

Sina uhakika kama itakufaa lakini mafanikio ni kile ambacho kinaweza kuendelea hata kama wewe mwenyewe haupo.

Kwa mfano, una biashara ambayo inajiendesha yenyewe ambayo imeajiri watu wengi kwa mfano 1000 hayo ndiyo mafanikio.

Mafanikio ni kuwa na mchango kwa watu wengine na watu wananufaika na kile ulichofanya hata kama haupo.

Watu wengi wanafanya kazi au biashara lakini bila wao kuwepo hakuna hela inayoingia kwanini? Kwa sababu biashara hazina mfumo wa kujiendesha. Mtu akitaka hata kwenda sehemu hana uhuru analazimika afunge.

Watu wengi wanaofariki na walikuwa na biashara wanakuwa kama wana laana fulani, yaani wakifa na biashara zao zinakufa kwa sababu gani? Kwa sababu hawajaweza kujenga biashara ambazo zina mifumo inayojiendesha yenyewe pasipo hata uwepo wao.

Kwa mfano rahisi sana mchukulie mtu kama Marehemu Reginald Mengi yule alikuwa amefanikiwa hayupo lakini biashara zake zote zinafanya kazi, amekufa lakini jina lake bado linaendelea kuishi kama kawaida.

Pata picha ameajiri watu wangapi? Ni wangapi wanaendesha maisha yao kupitia yeye.

Isifikie mahali ukajisifu na vitu ambavyo havina mchango kwa dunia, bali kwa familia yako tu.

Hatua ya kuchukua leo; Fanya kitu ambacho kitaendelea kufanya kazi hata kama wewe haupo duniani.

Ukifa dunia itaendelea kunufaika na wewe siku zote, unakuwa haupo kimwili lakini kila siku unagusa maisha ya watu kupitia kile ulichoacha.

Siyo unakufa halafu na vile ulivyoanzisha navyo vinakufa kwa kukufuata nyuma, natumaini unayo mifano mizuri kwenye jamii yako ni wangapi walikuwa na biashara lakini baada ya wao kufa kila kitu kikapotea.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: