Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Rahisi Ya Kuwapoteza Wateja Wako

Uwe unafanya biashara au hufanyi lakini kiasili kila mtu ana mteja wake kwa sababu kuu moja ambayo ni kila mtu ni muuzaji.

Kwa sababu kama huna unachouza utayaendeshaji maisha yako? Wako wanaouza huduma, ujuzi, maarifa, uzoefu, muda nk.

Kitu muhimu sana wewe kama muuzaji unachotakiwa kufanya ni kutimiza ahadi unazotoa.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanawadanganya wateja wao kama vile watoto wadogo. Mteja siyo mtoto mdogo, ukimwahidi kitu, tafadhali tekeleza.

Na kama huwezi kutekeleza yale unayoahidi, usiahidi kitu.

Njia rahisi ya kuwapoteza wateja kwenye biashara au mahusiano na wengine ni kuahidi vitu halafu usivitekeleze.

Jijengee sifa nzuri kwenye biashara yako na maisha kiujumla kwa kuwa mtekelezaji wa kila unachoahidi.

Kwa kufanya hivyo, wateja na watu wengine watakutegemea na kukuamini.

Linda sana sifa ya uaminifu, ukiaminika kwa kitu fulani hakikisha unawapa walengwa kama wanavyotarajia kupata.

Hatua ya kuchukua leo; ahidi makubwa na tekeleza.

Kama huwezi kutekeleza usiahidi. Usione aibu kutokuahidi, hii inakuja kuwasumbua watu wengi kweli kwenye jamii zetu wanapenda kuahidi kwa hisia halafu baadaye wanashindwa kutekeleza ahadi hizo.

Sehemu yoyote ile usiahidi ukiwa na hisia yoyote ile iwe furaha au huzuni. Ahidi kwa kutumia akili wakati hisia ziko chini na fikra ziko juu.
Hisia zikiwa juu, uwezo wa mtu kufikiri na kufanya maamuzi unashuka.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: