Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Umepanda Gari Sahihi

Unapata wasiwasi gani wa safari?

Kwa mfano, umepanda gari lako la kwenda Arusha, lakini ukiwa kwenye gari unaanza kujiuliza sasa mbona Arusha hatufiki?

Kama umepanda gari sahihi usiwe na wasiwasi utafika kule unakokwenda.

Hii ina maana kwamba, ukikaa kwenye mchakato sahihi wa kufanya kitu fulani usiwe na wasiwasi na matokeo.

Kwa sababu matokeo mazuri yatakuja yenyewe kama umekaa kwenye mchakato sahihi.

Wako watu wengi wanafanya kazi, huduma au biashara fulani lakini wana wasiwasi na vile wanavyofanya kwa sababu hawaoni matokeo mazuri kwa haraka.

Kwenye kile unachofanya jichukulie umepanda gari la kwenda sehemu fulani, usiwe na wasiwasi utafika safari yako, jichukulie uko kwenye mchakato wa safari na wewe tulia kwenye gari na hatimaye utafika kule unakotaka kufika.

Wako wengine baada ya kuona hawafiki, wanashuka na kutaka kupanda gari lingine na kuona labda lile walilopanda siyo sahihi. Hapo ni mtu anaacha kufanya kile anachopaswa kufanya na kukimbilia fursa mpya anayosikia inalipa.

Usihangaike na mambo mengi yatakuja kukupoteza, tulia na kitu kimoja mpaka uone matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo; usitawanye nguvu zako kwa kuhangaika na kila fursa mpya unayoisikia, kaa na tulia kwenye kitu kimoja mpaka uone matokeo yake.

Haijalishi unapata matokeo gani sasa, wewe kaa kwenye mchakato sahihi na mambo mazuri yatakuja. Kumbuka shoka moja haliangushi mti, bali mkusanyiko wa mashoka ndiyo unaangusha mti.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: