Acha Kauli Hii Inayokufunga Kupata Muda Zaidi

Tunaishi kwenye zama ambazo kila mtu yuko 'bize" na mambo ya kufanya ni mengi kuliko muda tulionao. Tukisema tufanye kila kitu, hatutakuwa na muda wa kufanya lakini tunao muda wa mchache wa kufanya yale muhimu tu na siyo kila kitu. Mwanafalsafa Seneca aliwahi kunukuliwa akisema, “Siyo kwamba hatuna muda, bali tuna muda mwingi mpaka tunaupoteza …

Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha

Ukiwa unataka kujua vitu vingi, basi jifunze sana na ishi kwa unyenyekevu kama vile hujui kitu. Kubali kuwa mwanafunzi wa maisha na utajifunza vitu vingi. Watu wako tayari kukufundisha pale unapokuwa tayari lakini ukijifanya mjuaji watu watakuacha uangamie. Huwezi kuwa bora kwenye kila kitu, kila mtu ana ubora wake kwenye eneo fulani la maisha yake. …

Usikubali Kufanya Kitu Hiki

Rafiki yangu, Kwa chochote kile unachofanya,Usikubali kufanya kitu kitakachodumu kwa muda mfupi, kwa msimu, tu kisha kikapotea. Fanya kazi itakayodumu muda mrefu, itakayodumu vizazi na vizazi. Tengeneza kitu ambacho kitaishi kwa muda mrefu kuliko muda utakaoishi wewe.Na kwa kufanya hivyo, ndivyo dhana ya wewe kuishi milele. Leo hii tunatumia kazi za watu wengi ambao walishaondoka …

Kitu Cha Kutegemea Kwa Binadamu

Ni mabadiliko. Unapokuwa na mtu yeyote yule mpe nafasi kwamba iko siku atakuja kubadilika na ukishajiandaa hivyo kisaikolojia na likija kutokea kweli halitakuumiza. Unapaswa uishi falsafa ya ustoa, unapaswa kutegemea mambo kwenda tofauti na unavyotarajia. Unapaswa kutarajia kwamba watu wanabadilika, hivyo kuwa tayari kupokea chochote kile kutoka kwa mtu hata ambaye ulikuwa hutarajii kama anaweza …

Je, Wewe Ni Nani?

Kama bado hujafungua ndoa na utajiri na kuupa umasikini talaka, jipatie nakala yako leo kwa bei ya ofa shilingi elfu 5 badala ya elfu 10 ili uweze kupata maarifa sahihi yatakayokuwezesha kufunga ndoa na utajiri na kuupa umasikini talaka. 0717101505 Inasikitisha kuona watu ambao wanataka kupata mafanikio pasipo kufanya kazi. Wako ambao wanaamini kwa njia …

Usiangalie Maumivu Unayopitia Bali Angalia Hiki Hapa

Jiunge na Klabu ya Mimi Ni Mshindi Nimezaliwa Kushinda ili upate maarifa sahihi yatakayokuwezesha kupiga hatua kwenye kile unachofanya. Kiasili sisi binadamu ni watu wa kukata tamaa, kuchoka, kuahirisha mambo. Pale mambo yanapokwenda kinyume na sisi tunaruhusu hali za kushindwa. Watu huwa hawapendi kujitesa, hata katika kazi mtu akiona kazi au kile anachofanya kinamchosha anaamua …

Bado Hujamaliza Kazi

Pata nakala yako leo kwa bei punguzo shilingi elfu 5. Usikubali kuishi bila kujua sababu za kwanini umezaliwa kushinda Huwa tunaona tumeshafika kwenye baadhi ya maeneo katika maisha yetu. Tunaona tumemaliza kazi na hatuna tena cha kutuhangaisha kuweka kazi. Kifupi ni kwamba bado hujamaliza kazi, unaweza ukajiambia kwa sasa umemaliza kazi kwenye kutafuta masoko eneo …

Fuata Moyo Wako

Mara nyingi sisi binadamu huwa tunapata ishara mbalimbali kupitia miili yetu juu ya kitu fulani kutokea. Kwa mfano, unaweza kukutana na mtu ambaye si salama kwako, kwa kumuangalia tu mwili wako unasisimka na kukupa ishara kwamba mtu fulani siyo salama. Ni muhimu sana kuheshimu ishara tunazopata. Heshimu machale unayopata kupitia vitu mbalimbali kwenye maisha yako. …

Jiongeze

Pale mambo yanapokuwa yanaonekana hayapo sawa kwenye kila eneo la maisha yako, unatakiwa kujiongeza kwa kuchukua hatua sahihi. Kwa mfano, gharama za maisha zimepanda, kila kitu kipo juu, kuendelea kulalamika siyo ujanja bali ni ujinga kwani malalamiko yako hayatakusaidia. Kumbe basi, unachotakiwa kufanya baada ya kuona hali ya maisha kuwa ngumu ni kujiongeza. Unajiongezaje kwa …

Jinsi Ya Kumpandisha Bei Mwenza Wako

Kadiri ya uzoefu wangu wa kujifunza na huduma ninayotoa kwenye eneo la mahusiano na yale ninayokutana nayo kwenye jamii nimekuja kuona kwamba baadhi ya Wanandoa wanashushana bei. Inakuwaje mpaka mtu anamshusha bei mwenza wake? Ni pale mwenza anapokuwa hampi mwenza wake thamani anayostahili kupata. Kwa mfano, kumsema mwenza wako kwenye kadamnasi huko ni kumshusha bei. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started