Design a site like this with WordPress.com
Get started

Bado Hujamaliza Kazi

Pata nakala yako leo kwa bei punguzo shilingi elfu 5. Usikubali kuishi bila kujua sababu za kwanini umezaliwa kushinda

Huwa tunaona tumeshafika kwenye baadhi ya maeneo katika maisha yetu. Tunaona tumemaliza kazi na hatuna tena cha kutuhangaisha kuweka kazi.

Kifupi ni kwamba bado hujamaliza kazi, unaweza ukajiambia kwa sasa umemaliza kazi kwenye kutafuta masoko eneo fulani lakini ukweli ni kwamba bado hujamaliza kazi. Bado kuna wateja wengi tu kwenye eneo lako hawajui kuhusu biashara yako. Bado hujamaliza kazi ya kuwapitia wateja wako wote, huwa tunajidanganya kwamba tumemaliza kazi kumbe kazi inahitajika.

Kwenye maisha ni kama kuendesha baiskeli, usipopiga pedeli baiskeli haitoenda itaishia kusimama na kuanguka chini. Hata wewe kwenye maisha yako, isifikie mahali useme sasa nimemaliza kazi.

Bado hujamaliza kazi unahitaji kuendelea kuweka kazi zaidi kwenye kile unachofanya. Kwenye kujifunza zaidi, bado hujamaliza kusoma vitabu vingi na mpaka unaondoka duniani hutaweza kuvimaliza, hivyo endelea kujifunza.

Kuwa na msaidizi wa kazi siyo kwamba umeamaliza kazi bado unahitaji kuweka kazi ya uangalizi na kufuatilia namna kazi yako inavyokwenda. Kuajiri siyo kumaliza kazi bado unahitaji kuweka juhudi kwenye kufuatilia kile unachofanyiwa.

Popote pale ambapo fedha zako zipo hakikisha macho yako yanakuwa pale kwa ufuatiliaji wa karibu.

Kwenye kila eneo la maisha yako, bado unao uwezo wa kuboresha zaidi kile unachofanya. Maboresho hayana ukomo, kila siku weka kazi na angalia namna ya kuboresha zaidi na usiseme umemaliza kazi.

Maisha yetu ni kazi ya sanaa na kazi ya sanaa haina ukomo katika ubunifu. Pale unapoona unaweza kufanya kitu na kuwa bora zaidi fanya kuliko kufikia hali ya mazoea kuona kama vile umemaliza kazi.

Unaweza ukajiona umemaliza kazi kwa njia ya kufanya kwa mazoea lakini pale unapoondoa mazoea na kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako utajiona wazi bado hujamaliza kazi. Kwa mfano, kazi, ndoa, biashara na mahusiano kwa ujumla ukifanya kwa mazoea utajiona umemaliza kazi lakini ukweli ni kwamba bado hujamaliza kazi.

Hatua ya kuchukua leo; jiambie bado hujamaliza kazi kwenye kila eneo la maisha yako. Unahitaji kuweka kazi zaidi kuliko ulivyozoea kufanya.

Nenda hatua ya ziada, usikubali kupata matokeo ya kawaida kwa kujiambia umemaliza kazi eneo fulani la maisha yako bado kazi inahitajika zaidi ili uweze kufanikiwa kwenye kile unachotaka.
Bado hujatumia uwezo wako wote mkubwa ulionao halafu unasema umemaliza kazi? Tumia silaha zote ulizokuwa nazo kuhakikisha unakuwa bora.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: