Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jiongeze

Pale mambo yanapokuwa yanaonekana hayapo sawa kwenye kila eneo la maisha yako, unatakiwa kujiongeza kwa kuchukua hatua sahihi.

Kwa mfano, gharama za maisha zimepanda, kila kitu kipo juu, kuendelea kulalamika siyo ujanja bali ni ujinga kwani malalamiko yako hayatakusaidia.

Kumbe basi, unachotakiwa kufanya baada ya kuona hali ya maisha kuwa ngumu ni kujiongeza. Unajiongezaje kwa mfano? Kwa kuongeza kipato zaidi. Kama gharama za maisha zimepanda, jiongeze na wewe panda kwa kuongeza kipato chako ili uweze kuzikabili gharama za maisha.

Unapoona wengine wanapiga hatua jiongeze na wewe kwa kwenda kuwauliza, je, unatumia mbinu gani zinazokuwezesha kufanikiwa kwenye kitu fulani?

Jiongeze kwa kuwa na maarifa sahihi yatakayokuwezesha kuimarisha mahusiano yako lakini pia kujenga ushawishi.

Jiongeze namna ya kufanya kazi yako vizuri.

Jiongeze namna ya kufanya biashara yako.

Jiongeze namna ya kufanya masoko, kupata wateja kwenye biashara yako na kisha wateja kufanya manunuzi.

Hatua ya kuchukua leo; nenda kajiongeze kwa kuchukua hatua sahihi kwenye kile ambacho unajua kabisa hauko sawa.
Chukua hatua sasa ili uwe vizuri.

Maisha ni kujiongeza, siyo kusubiri kuambiwa kila kitu. Unapoona kitu hakipo sawa jiongeze haraka na kwenda kukiweka sawa.

Bila kujiongeza kwenye kila eneo la maisha yako, utaendelea kubaki hivyo ulivyo.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: