Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kumpandisha Bei Mwenza Wako

Kadiri ya uzoefu wangu wa kujifunza na huduma ninayotoa kwenye eneo la mahusiano na yale ninayokutana nayo kwenye jamii nimekuja kuona kwamba baadhi ya Wanandoa wanashushana bei.

Inakuwaje mpaka mtu anamshusha bei mwenza wake? Ni pale mwenza anapokuwa hampi mwenza wake thamani anayostahili kupata. Kwa mfano, kumsema mwenza wako kwenye kadamnasi huko ni kumshusha bei.

Lakini pale unapomsifia na kumpongeza kwa mazuri anayofanya ni kumpandisha bei mwenza wako.

Kumpatia heshima mwenza wako ni kumpandisha bei na siyo kumshusha.

Angalia matendo unayomfanyia mwenzako wa ndoa ni ya kumpandisha bei au kumshusha bei?

Fanya yale mambo ambayo yatampandisha bei mwenza wako wa ndoa na kuonekana wa thamani na siyo vinginenvyo.

Jua njaa ya mwenza wako na kisha mshibishe kwa kufanya hivyo utakua umempandisha bei.

Kuongea vizuri na mwenza wako mbele ya watu ni kumpandisha bei lakini kuongea lugha mbaya mbele ya watu ni kumshusha bei mwenza wako.

Kumtukana mwenza wako ni kumshusha bei hivyo pandisha bei ya mwenza wako kwa kutomfedhehesha na kumzalilisha.

Hatua ya kuchukua leo; mpandishe bei mwenza wako kwa kumtendea yale anayopaswa kutendewa kama mwenza wako.

Kwahiyo, wewe ndiyo wa kuishusha au kuipandisha thamani ya mwenza wako.
Jitafakari, je yale unayofanya yanampandisha au yanamshusha bei mwenza wako?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: