
Ni mabadiliko.
Unapokuwa na mtu yeyote yule mpe nafasi kwamba iko siku atakuja kubadilika na ukishajiandaa hivyo kisaikolojia na likija kutokea kweli halitakuumiza.
Unapaswa uishi falsafa ya ustoa, unapaswa kutegemea mambo kwenda tofauti na unavyotarajia.
Unapaswa kutarajia kwamba watu wanabadilika, hivyo kuwa tayari kupokea chochote kile kutoka kwa mtu hata ambaye ulikuwa hutarajii kama anaweza kukuangusha kwenye kitu fulani.
Tabia ya binadamu ni kubadilika, hivyo usishangazwe pale unapoona mtu amebadilika.
Binadamu siyo mti, useme utakapouacha ndipo utakapoukuta. Tegemea watu kubadilika na watakapobadilika jiambie tu uliju watabadilika.
Kila kitu kinabadilika kwenye maisha, kuwa tayari kujifunza na kuendana na mabadiliko unayopokea na kukutana nayo.
Hatua ya kuchukua leo; tarajia kuona mabadiliko lakini pia tarajia kuona watu wanabadilika, hali ya kazi, biashara unayopitia sasa itabadilika kwani hakuna hali ya kudumu kwenye maisha, kila kitu kinatokea kwa sababu ya kukupa somo fulani.
Kwenye maisha hakuna kusimama, kama huendi mbele basi jua unarudi nyuma. Fanya mabadiliko ili uende mbele kama unaona unarudi nyuma.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog