Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiangalie Maumivu Unayopitia Bali Angalia Hiki Hapa

Jiunge na Klabu ya Mimi Ni Mshindi Nimezaliwa Kushinda ili upate maarifa sahihi yatakayokuwezesha kupiga hatua kwenye kile unachofanya.

Kiasili sisi binadamu ni watu wa kukata tamaa, kuchoka, kuahirisha mambo. Pale mambo yanapokwenda kinyume na sisi tunaruhusu hali za kushindwa.

Watu huwa hawapendi kujitesa, hata katika kazi mtu akiona kazi au kile anachofanya kinamchosha anaamua kuacha na kutafuta kitu ambacho hakina maumivu.

Kwenye maisha hakuna kitu ambacho utakipata bila maumivu. Najua unapata shida kupata kile unachotaka na wakati mwingine unachoka na unaona ni sahihi kabisa kwako kama binadamu kukata tamaa na kutokuendelea na kile unachofanya.

Ukiwa unaangalia maumivu unayopitia hakika ni rahisi sana kuishia njiani. Lakini ukiangalia manufaa unayopata kupitia kile unachofanya basi yale manufaa huwa yanafuta maumivu yote.

Pale unapopitia maumivu makubwa unatakiwa ujipe hamasa zaidi ya kusonga mbele, uyafute maumivu yote kwa kuangalia ni manufaa gani unayopata kupitia kile unachofanya.

Wengi wanaishia njiani kwa sababu ya maumivu wanayopata wakati wa mapambano. Unapokuwa katika maumivu makali vumilia na ona unakaribia kupata kile unachotaka.

Kwa mfano, kuandika kitabu au kuandika kila siku ni kazi inayochosha. Kama ningekuwa naangalia maumivu ningeshaacha siku nyingi lakini naangalia manufaa yanayopatikana. Kuna watu wanategemea kile nilicho nacho, na sisi kazi yetu ni kutoa basi sina budi kutoa iwe napitia maumivu au la kwani napoangalia manufaa maumivu yanaondoka yenyewe.

Hakuna kitu ambacho ni rahisi kwenye hii dunia, kazi ambayo ni rahisi ni kuongea, kukosoa na kuchambua. Kwa mfano, waangalie wale wanaochambua mpira wa miguu, wanaongea kirahisi kweli lakini hawajui ni jinsi gani wale wanaocheza wanavyopitia maumivu.

Waheshimu wale walioweza kufanya kitu hata kama wewe unakidharau lakini wapongeze kwa sababu hakuna kitu kirahisi. Kabla hujakosoa jiulize ni kipi kikubwa ambacho wewe umefanya?

Hatua ya kuchukua leo; Usiangalie maumivu unayopitia, bali angalia manufaa ambayo unakwenda kupata.

Kwa mfano, mchakato wa kupata kitu chochote kile huwa unakuwa mgumu, lakini ukiwa unaangalia maumivu ya mchakato unayopitia ni rahisi kuishia njiani lakini wewe angalia baada ya maumivu nini unakwenda kupata?

Manufaa unayopata yanafuta maumivu unayopitia. Usiangalie maumivu unayopitia bali angalia manufaa unayopata na hii itakusukuma kufika mbali.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: