Design a site like this with WordPress.com
Get started

Fuata Moyo Wako

Mara nyingi sisi binadamu huwa tunapata ishara mbalimbali kupitia miili yetu juu ya kitu fulani kutokea.

Kwa mfano, unaweza kukutana na mtu ambaye si salama kwako, kwa kumuangalia tu mwili wako unasisimka na kukupa ishara kwamba mtu fulani siyo salama.

Ni muhimu sana kuheshimu ishara tunazopata. Heshimu machale unayopata kupitia vitu mbalimbali kwenye maisha yako.

Fuata moyo wako, angalia kile ambacho moyo unataka lakini kiwe sahihi kufanya. Wako ambao wanafuata mioyo yao lakini wakati mwingine siyo kila ambacho moyo wako unakuambia kitakuwa ni sahihi unapaswa kuwa makini hapo.

Wengine wanasema ni machale na wengine wanasema kiroho ni roho mtakatifu anakuwa anakupa ishara ya kitu kabla haijatokea. Kwa mfano, ndugu mmoja alikuwa stand na mke wake wakisubiria gari kwa ajili ya kwenda mjini, mara nyingi huwa kuna gari ambalo huwa wanapendelea kupanda.
Sasa gari lile likapita lakini Yule ndugu akamwambia mke wake, leo tusipande gari hili tubadilishe moyo wangu hautaki kabisa kupanda hili gari na wakaliacha liende.

Baadaye wakapanda gari lingine, wanafika mbele kidogo wakakuta lile gari ambalo walipaswa kupanda limepata ajali na watu wengi kufariki.

Hapo tunajifunza nini? Kusikiliza sauti yako ya ndani inakuambia nini, kusikiliza moyo wako, kusikiliza machale, au kusikiliza roho mtakatifu anakuambia nini.

Mara nyingi huwa tunapotezea hizi ishara au machale mbalimbali tunayopata lakini baadaye yanakuja kutokea kweli.

Wakati mwingine miili yetu inatupa ishara hata ya kifo hata kama mtu hajakuambia wewe mwenyewe unakuwa unahisi juu ya kitu fulani kabla hata hujaambiwa.

Hatua ya kuchukua leo; tumia machale unayopata au ishara mbalimbali unazopata kupitia mwili wako na usizipuuze bali zilifanyie kazi.

Hujawahi kutaka kwenda kwa mtu lakini unapata ishara kwamba ukienda hutamkuta mhusika na baadaye ukija kumuuliza atakuambia ni kweli hakuwepo.

Au unataka kumuomba mtu kitu fulani ndani yako umeshakuwa na majibu kwamba mtu fulani atakupatia au la.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: