Kosa Ambalo Wauzaji Wengi Huwa Wanalifanya Kwenye Biashara

Unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kama utaweza kuuza zaidi. Ni kweli hilo halina ubishi, mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara na maisha kiujumla. Mauzo ndiyo moyo wa biashara, ambapo yanasukuma damu ya biashara ambayo ni fedha. Bila mauzo hakuna fedha kwenye biashara, na bila fedha hakuna biashara. Unaona hapo mauzo yalivyokuwa muhimu? …

Siri Namba Moja Ya Kupata Fedha

Kwenye kitabu cha The Baron letters, mwandishi Gary Halbert alimwandikia barua mtoto wake akiwa gerezani. Gary Halbert alikuwa mwandishi bora kabisa wa matangazo na hivyo alitumia muda wake kumshirikisha mtoto wake yale yote aliyojifunza kwenye maisha, kuanzia kuwa na afya bora, kupata nk. Hata wewe kama ni mzazi unaweza ukawa unaandika yale uliyojifunza na kumshirikisha …

Una Uhakika Wa Kufanikiwa

Sina uhakika kama itakufaa lakini ukichagua kitu kimoja au vichache ambavyo utavifanya kwa maisha yako yote, ukawa unajifunza kila siku na kuchukua hatua, halafu ukaachana na mengine yote wanayofanya wengine,Una Uhakika Wa Kufanikiwa. Watu wengi hawajatulia kwenye kitu kimoja, wamekuwa wanahangaika na kila jambo linalokuja mbele yao. Na mwisho wa siku wanakuwa wamechoka kweli lakini …

Ufunguo wa Kushindwa

Bill Cosby aliwahi kunukuliwa akisema, sijui ufunguo wa mafanikio ni upi, lakini ufunguo wa kushindwa ni kujaribu kumridhisha kila mtu. Sidhani kama nitakuwa na maneno mengine zaidi ya hayo. Ukitaka kushindwa kwenye maisha yako, basi jaribu kumridhisha kila mtu. Na ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako ishi vile utakavyo lakini usivunje sheria za asili na za …

Miaka 200 Ijayo

Kuwa na kiasi kwenye maisha yako, haijalishi umefanikiwa kiasi gani miaka 200 ijayo huenda hakuna atakayejua hata kama uliishi hapa duniani. Kila unapoanza kujiona wewe ni muhimu kuliko wengine kumbuka kitakachotokea MIAKA 200 ijayo na dunia itakua imekusahau kabisa. Rafiki, ishi maisha yenye maana kwako na siyo maisha ya kujionesha na kutaka wengine waone wewe …

Jinsi Ya Kuondokana Na Wivu

Maana rahisi ya wivu ni kujiona wewe unastahili zaidi kuliko wengine. Sina uhakika kama itakufaa, na wivu ni wivu tu, hakuna wivu mzuri wala mbaya. Jinsi gani ya kuondokana na wivu? Usiwe na wasiwasi utapata majibu sahihi hapa. Kwanza ni rahisi sana, usijilinganishe na yeyote. Pili, kubali kwamba kuna watu watakaokuwa wamekuzidi kwa chochote unachofikiri …

Pata Picha Leo Unaacha Kuwa Hivi

Kama ulikuwa haujui, akili zetu sisi binadamu ni volkano ya maoni. Kwa nini? Kwa sababu tunapenda kuwa na maoni kwenye kila kinachotokea aidha tunakijua au hatukijui ndiyo maana ukiwaomba watu maoni hata hana atajilazimisha kusema tu maana asipofanya hivyo watu watamuonaje au watamchukuliaje. Wanafalsafa wengi wanatuambia siyo sahihi kuwa na maoni kwenye kila kitu. Kama …

Hiki Ni Kitu Cha Uhakika Kwenye Maisha Yako

Sina uhakika kama itakufaa lakini leo nina habari njema kwako rafiki yangu nikupendaye. Moja kuwa tayari kupoteza kila kitu. Na uwe uhuru kupoteza kila kitu wala usitetereke kwa kwenye maisha kuwa huru ina maanisha kuishi utakavyo na kupata unachotaka. Mbili, chochote kile ulichonacho kwenye maisha yako utakipoteza huo ni uhakika wala halihitaji ubishi. Hiyo ni …

Maisha Bora Ni Kufanya Vitu Hivi

Vitu tunavyofanya kwenye maisha yetu vina pande mbili; Moja raha naMbili maana. Tunasukumwa kufanya vitu kwa sababu labda vina raha kwetu kufanya au vina maana kwetu. Maisha bora ni kufanya vitu ambavyo vina raha na maana na siyo kuegemea upande mmoja pekee. Kuna wakati unahitaji kufanya vitu vya raha na ukijisikia kufanya hivyo fanya kwa …

Kabla Hujampenda Mtu Yeyote Mpende Kwanza Huyu

Jipende kwanza wewe mwenyewe. Mtu anayefanya vizuri kwenye eneo lolote lile ni yule ambaye anaanza kujipenda yeye mwenyewe kwanza. Unapojipenda wewe mwenyewe kwanza, itakulazimisha hata wale waliokuzunguka wawe bora na wajipende wao wenyewe. Kwa sababu, hatuwezi kuwabadilisha watu wawe vile tunavyotaka sisi pasipo sisi kuwaonesha kwa vitendo. Hatuwezi kuwapenda wengine kama sisi wenyewe hatujipendi. Falsafa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started