Waswahili wanasema, liwezekanalo leo lisingoje kesho. Kuna mtu mmoja alisema, “kusitasita ni chanzo cha matatizo yangu yote. Hata hivyo sijui maana ya neno kusitasita kesho nitatazama maana yake kwenye kamusi” Hapa tunaona ni jinsi gani mtu huyu alikuwa bado na tatizo la kusitasita. Maadui wa kutumia fursa za leo ni kusitasita na kuahirisha mambo. Hebu …
Category Archives: Uncategorized
Jinsi Ya Kupata Majibu Sahihi
Kama unataka kupata majibu sahihi. Uliza maswali sahihi. Anayeuliza mengi anajifunza mengi na kubaki na mengi. Asiyeuliza hajifunzi. Kuna vitu vingi huvijui lakini unaona wengine wanajua uliza ili ujue usikae kimya. Kuuliza si ujinga bali ni ujanja. Kile unachopenda lazima utapata muda wa kukifurahia. Lakini pia kile unachopenda lazima utapata muda wa kujifunza na kuuliza …
Hiki Ndiyo Kitu Unachoweza Kuchagua Kuweka Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako
“Mawazo ya wenye bidii huelekea utajiri tu, bali kila mwenye pupa huelekea uhitaji” alisema mwandishi wa kitabu cha Mithali. Katika kila jambo kuhitaji bidii. Bidii ni nguvu iwezeshayo mtu kufikia malengo yaliyo mbele yake. Kitu hicho ni bidii. Chagua kuweka bidii kwenye kazi na utafanikiwa sana. Chagua kuweka bidii kwenye ndoa, mahusiano yako kwa ujumla …
Continue reading “Hiki Ndiyo Kitu Unachoweza Kuchagua Kuweka Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako”
Hii Ndiyo Hatua Ngumu Kuliko Zote
Umbali si hoja, hatua ya kwanza ndiyo ngumu aliwahi kusema Mari de Vichy-Chamrond Marquise du Deffand. Ukitaka kufika mbali fanya juhudi ya kuanza tu. Usiangalie umbali unaotakiwa kufika bali wewe angalia hatua moja unachokua kila siku. Mwanzo ni mgumu kweli, lakini jaribu kupiga hatua ya kwanza na ugumu utaondoka wenyewe. Kuchukua hatua ya kwanza ni …
Nenda Leo Kaandike Historia Hii Hapa Muhimu Kwenye Maisha Yako
Huwa ni kawaida ya binadamu kuandika historia. Wengine wanaandika historia nzuri na wengine historia mbaya. Tumekuwa siyo watu wa kuandika historia nzuri za maisha yetu ya kiroho. Leo ninakusihi sana ondoka hapo ulipo na nenda kamwambie mtesi wako nisamehe nimekosa. Historia nzuri unayopaswa kuiacha leo ni wewe kwenda kumsamehe yule aliyekukosea. Huna haja ya kumsubiria …
Continue reading “Nenda Leo Kaandike Historia Hii Hapa Muhimu Kwenye Maisha Yako”
Huwezi Kutenganisha Vitu Hivi Viwili
Watu wengi wanatumia nguvu kutenganisha kati ya jina, tabia na mtu. Huwezi kutenganisha jina lako na tabia yako. Kwa mfano, wewe unaiba halafu unalazimisha uitwe muungwana na badala ya mwizi. Tabia hutenganisha jina la kweli la mtu. Ukitaka kuitwa mwalimu basi uwe na tabia za kweli za mwalimu. La sivyo watu watakudharau kukuita mwalimu, wakati …
Njia Rahisi Ya Kujibariki
Jibariki kwa maneno yako mwenyewe. Kiasili wewe tayari umezaliwa na baraka kwani baraka ni nguvu ya asili kutoka kwa Mungu inayofanya kazi ndani yako. Kwa kujua au kwa kutokujua. Maneno yana nguvu sana.Yanaweza kujenga au kubomoa. Yanaweza kubariki au kulaani. Waswahili wanasema, neno litokalo halirudi. Hii ni methali ya kiswahili. Ni sawa na kusema kwamba …
Uhakika Wa Ushindi Utakuwepo Endapo Kitu Hiki Kitakuwa Kimefanyika
Endapo kazi itakuwa imefanyika. Hakuna uhakika wa ushindi kama kazi haijafanyika. Usijiwekee uhakika wa kupata ushindi wakati huna kazi uliyoweka. Uhakika wa kupata kile unachotaka ni kazi uliyoweka juu ya ushindi unaotaka. Ukifanya kazi lazima utapata uhakika. Kwa kazi hii niliyofanya lazima nitapata ushindi. Je, una uhakika wa kupata ushindi wowote ule leo? Kama jibu …
Continue reading “Uhakika Wa Ushindi Utakuwepo Endapo Kitu Hiki Kitakuwa Kimefanyika”
Usiseme Haliwezekani Kufanyika
Kama kuna kitu huwezi, kaa pembeni waachie wanaoweza kufanya. Fanya kile unachoweza na usichokiweza waachie wanaoweza kufanya kazi hiyo. Ukisema huwezi, kuna watu wanaweza. Albert Hubbard aliwahi kusema, dunia inakwenda haraka sana siku hizi mtu anaposema haliwezekani kufanyika kwa kawaida anakatizwa na mtu anayelifanya. Dunia inakwenda kwa kasi, unachosema hakiwezekani kinawezekana. Huenda hakiwezekani kwako tu …
Kumdunisha Mwingine Ni Kujidunisha Wewe Mwenyewe
Kile tunachofanya kwa wengine kiwe kizuri au kibaya lazima kiturudie kwa namna yoyote ile. Kwa sababu, asili huwa ina tabia ya kumlipa mtu kwa kile anachotoa kiwe kizuri au kibaya. Kuwa makini sana kile unachowafanyia wengine. Kumdhalilisha mtu mwingine ni kujidhalilisha. Kwani watu watajiuliza watajisemea moyoni kama ameweza kuyasema ya wengine namna hii vipi mimi …
Continue reading “Kumdunisha Mwingine Ni Kujidunisha Wewe Mwenyewe”