Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Matokeo Ya Kutosema Ukweli Wa Mambo

Usiposema ukweli wa mambo, watu watatunga hadithi wanazojua wao.

Kama familia, kikundi, taasisi au kampuni jambo linapotokea liwekeni wazi kabla watu hawajaanza kusema yale ambayo hayapo.

Unapoweka ukweli hadharani, watu wanashindwa kutengeneza hadithi mpya. Lakini, ukificha mambo usipotoa taarifa watu watabaki njia panda na hapo ndipo wanaamua kusema vitu ambavyo haviko.

Usisubiri mpaka watu watengeneze hadithi ambazo siyo kweli na wewe ndiyo utoe ukweli.

Wale wanaotakiwa kupata ukweli, waambie mapema nini kinaendelea aidha katika familia, taasisi au kampuni. Watu wakijua wanapitia nini ni rahisi kutonung’unika.
Ukiwa kimya bila kuwaambia watu ukweli watasema kile wanachojua wao. Ukishaweka mambo wazi hata mtu akija kutengeneza hadithi mpya itaonekana ni ya uongo.

Wewe kama ni kiongozi hakikisha unawapa mwanga kwa wale unaowaongoza kule mnakotoka na mnakoenda na hali mnayopitia.

Utasikia maneno ya chini chini kama uongozi haujaweka mambo wazi. Epusha usiri ili kuepuka kuleta taharuki.

Hatua ya kuchukua leo; Weka ukweli wa mambo wazi kwani usipofanya hivyo watu watatengeneza hadithi zao ambazo siyo kweli.

Kwahiyo, nenda kawe mkweli, muwazi na mwajibikaji.
Aliyekuwa raisi wa jamhuri wa Tanzania Hayati Mkapa alikuwa na falsafa yake katika uongozi ambayo ni ukweli, uwazi na uwajibikaji na wewe nenda kaitumie hiyo kwenye maisha yako itakusaidia kupata matokeo mazuri.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: