Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukiwahudumia Vizuri Watu Hawa Lazima Utafanikiwa

Tumeitwa kutumika na siyo kutumikiwa. Kila mmoja anaalikwa kuwatumikia watu na siyo kutumikiwa.

Yeyote unayekutana naye na anahitaji huduma kutoka kwako ukifanikiwa kumhudumia vizuri sana lazima utafanikiwa.

Ukiwahudumia vizuri wale wanaohitaji huduma kutoka kwako lazima utafanikiwa. Hakuna kingine kitakachokutoa hapo ulipo kama huna huduma bora.

Wale ambao wanategemea huduma kutoka kwako, hakikisha unawahudumia vizuri sana. Wape huduma bora ambayo hata wao wenyewe washangae.

Kama wewe umeitwa katika huduma ya kiroho, basi ponya roho za watu. Hakikisha unamtumikia Mungu kweli kiuaminifu. Acha mapenzi ya Mungu yatimie juu yako na siyo mapenzi ya binadamu.

Kama umeajiriwa toa huduma bora sana. Bosi wako ndiyo mteja wako wa kwanza hivyo anataka umpatie huduma bora ambayo anaitegemea kupata kutoka kwako.

Mteja wako anaacha sehemu nyingine zote na kuja wako. Mteja wako aendelee kuwa mfalme kwa kumhudumia vizuri sana. Kwa sababu yeye ndiyo anakufanya wewe maisha yako yaende. Bila mteja kwenye kile unachofanya huna unachofanya.

Mke au mume wako ni mteja wako hivyo hakikisha unajitoa kwa mteja wako. Mpatie huduma bora ambayo hataweza kuipata kwa mtu mwingine. Mteja anafurahia pale anapohudumiwa vizuri. Hivyo kama uko kwenye mahusiano ya ndoa hakikisha mume au mke wako anapata huduma bora kutoka kwako.

Usichukulie poa hili, mahusiano yanahitaji kazi yenye huduma bora. Watu wana njaa kwenye mahusiano ukifanikiwa kushibisha njaa yake vizuri utakuwa umefanikiwa kumbakisha kwenye himaya yako.

Kama una watoto pia wanahitaji huduma bora kutoka kwako mzazi. Watoto wahudumie vizuri, wape kile ambacho wanahitaji kutoka kwako. Usipowahudumia vizuri wako ambao watakuja kuwadanganya na kuwatumia watoto wako vile wanavyotaka wao. Wafundishe watoto wako yale ya msingi ili waishi katika misingi. Usipowapa watoto misingi, wataanguka kwa kitu chochote kile.

Kama wewe ni kiongozi wahudumie vizuri wale unaowaongoza. Kuwa mtumishi wa wote. Fanya kazi uliyopewa vizuri. Kuwa mwadilifu kwani uadilifu ni zawadi ghali ambayo huwezi kuipata kwa mtu wa kawaida.

Unapotoa huduma zingatia sana uaminifu, uadilifu na kujituma. Kisha toa huduma yako kwa kufuata upendo.

Hatua ya kuchukua leo; Akili yako muda wote iwaze kutoa huduma bora sana. Kwa sababu huduma bora ndiyo msingi wa mafanikio.

Wawezeshe wengine kupata kile wanachotaka kwenye maisha yao. Wapatie huduma bora ambayo itakwenda kutatua matatizo waliyokuwa nayo.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: