Kuna watu ambao wanapenda kujipa kazi ambayo hata siyo yao. Kazi yenyewe ni ya kuwa kiranja wa dunia kutaka kuwanyoosha watu.
Mtu anapokuwa kiranja wa dunia maana yake anataka mambo yaende kama vile anavyotaka yeye. Anataka watu waishi vile anavyotaka yeye.
Ukitaka dunia iende kama vile unavyotaka wewe hiko ni kitu ambacho hakiwezekani.
Unaweza kujitawala wewe mwenyewe lakini siyo mambo ya nje. Tawala hisia zako na yale yote ambayo yako ndani ya uwezo wako.
Usitake kujipa kazi ya ukiranja wa dunia utachoka. Dunia iko kama ulivyoikuta na utaondoka na kuiacha kama ilivyo.
Kupambana na mambo yaliyo nje ya uwezo wako ni kujipa kazi ya kuwa kiranja wa dunia na hutoiweza.
Usitake kuinyoosha dunia maana hutoweza zaidi ya kujinyoosha wewe mwenyewe.
Huwezi kumyoosha mke, mume, watoto, wafanyakazi wako wawe kama vile unavyotaka wewe.
Kwenye hii dunia ili usijisumbue na mtu ishi maisha yako na waache watu wengine waishi na wafanye kile wanachotaka wao.
Hatuwezi kuwataka wengine wawe kama sisi. Waache wengine waishi kama wao wanavyotaka na wewe ishi vile unavyotaka kadiri ya viwango ulivyojiwekea.
Hatua ya kuchukua leo; Waache watu waishi kama vile wanavyotaka wao.
Na wewe ishi vile unavyotaka wewe mwenyewe.
Ishi maisha yako, na waache watu wengine waishi kama vile wanavyotaka wao.
Usijipe kazi ya ukiranja wa dunia wa kutaka kuinyoosha dunia badala yake ishi maisha yako. Wapende watu kama walivyo na siyo kutaka kuwabadilisha.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo