Hamasa ni kichocheo kinachokufanya mtu uendelee kujisukuma na kufanya kile unachopaswa kufanya.
Watu wanaweza kwenda mbele wakiwa na hamasa au kurudi nyuma sana kwa kukosa hamasa.
Na binadamu ndivyo tulivyo bila hamasa hatujisukumi kufanya. Zawadi zimewekwa ili kuibua hamasa ndani yetu ya kufanya kazi kwa bidii zaidi.
Ni muhimu sana hamasa katika maisha yetu ya kila siku. Tukipoteza hamasa tumepoteza tumaini la kujisukuma kwenye yale tunayoendelea kufanya.
Mara nyingi huwa tunategemea kupongezwa na watu wengine pale tunapofanya vizuri kwenye jambo fulani. Lakini, binadamu wote hatuko sawa. Unaweza ukafanya vizuri sana lakini usione hata wa kukupongeza.
Usitegemee watu wa nje waje kukupongeza ili uchukue hatua.
Badala ya kuwategemea watu wa nje, jitumie wewe mwenyewe kujihamasisha na kujiambia maneno mazuri na hata kujinunulia zawadi.
Kile ambacho unategemea kufanyiwa na watu baada ya kufanya kazi fulani jifanyie mwenyewe. Jinunulie kile ambacho ulitamani watu wakupatie, jiambie yale ambayo ulipenda watu wakuambie.
Maisha yanahitaji hamasa ili uweze kuchukua hatua zaidi. Jitie moyo, jipe hamasa wewe mwenyewe kwenye kile unachofanya na utakua na nguvu ya uthubutu.
Hatua ya kuchukua leo; Jiambie yale maneno uliyokuwa unatarajia watu watakuambia pale unapofanya kazi nzuri.
Jinunulie zawadi au kile unachotaka kwenye maisha yako kama sehemu ya kujipongeza kwa sababu ya kufanya vizuri au kutimiza Malengo yako.
Usiwasubiri watu wengine waje wakuhamasishe kwa maneno au kwa zawadi. Anza kujihamasisha na wewe aliye ndani yako.
Ukifanya kazi nzuri hata wewe mwenyewe unafurahia sasa mtumie huyo wewe aliye ndani yako kufanya makubwa baada ya kujipongeza na kujihamasisha.
Ukifanya vizuri jipongeze na ukifanya vibaya jipe adhabu ya kujinyima kitu ambacho unakipenda kufanya kila siku. Kwa mfano, kama unapenda kuangalia TV, unajinyima kuangaika kwa sababu umeshindwa kufanya kile ulichopanga kufanya.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo