Kuna wakati unafikiria mpaka akili inachoka na kufikia ukomo.
Unaona kabisa hapa siwezi kufanya kitu.
Leo ninayo habari njema sana kwako. Ukifikia hali kama hiyo acha imani itawale. Acha Mungu achukue nafasi yake.
Hutakiwi kujitesa kwa kila kitu na hutakiwi kufanya kila kitu peke yako. Na siyo kila kazi ni yako. Kazi zingine siyo zako ziko kabisa nje ya uwezo wako.
Kuna kazi nyingine ni za asili. Wewe unatakiwa kufanya kazi yako na kuiachia asili ifanye kazi yake.
Kumbuka kuwa, njia zetu ni ndogo na njia za Mungu ni za juu sana. Na njia zetu siyo njia za Mungu.
Wakati mwingine kuna mambo huwa yanaachiliwa kwetu kwa makusudi fulani baadaye unakuja kutambua kwa nini jambo fulani lilitokea.
Ukifikia ukomo wa kutenda kibinadamu acha Mungu achukue nafasi yake.
Unayo matatizo yanayokuandama. Kuna kitu ambacho hakipo sawa pengine. Lipe muda jambo lako na litakuwa vizuri baada ya asili kufanya kazi yake.
Hatua ya kuchukua leo; Ukiona kitu kina kusumbua kipe muda kwani muda ndiyo muamuzi wa yote.
Muda ndiyo msema kweli wa mambo yote. Wale wanaokusumbua au vile vinavyokusumbua vipe muda.
Mwachie Mungu afanye kazi yake baada ya wewe kumaliza kazi yako.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo