Watu huwa wanalalamika juu ya vile wanavyofanya na vile wanavyofanyiwa.
Unaweza ukawa unafanya kazi sana watu wakakusema na kukuambia huchoki au hujionei huruma.
Usipofanya kazi watu watakuona mzembe na ukifanya kazi watu wanakuona wewe ni mtu unayejitesa. Sasa ufanye lipi? Fanya kazi.
Unajua kwa nini?
Kwa sababu; chochote kile unachofanya kama hakikuui basi, kinakuimarisha.
Ukiwa unasoma sana utaambiwa unaharibu macho yako achana na mambo ya kusoma.
Ukikutana na kitu ambacho wewe unapenda kukifanya halafu watu wanakuambia maneno ambayo huyaelewi wewe jiambie kwa kuwa hiki nachofanya hakiniui basi kitaniimarisha na kuwa bora.
Unapitia hali gani kwa sasa? Jiambie haikuui bali inakuimarisha kuwa bora.
Hatua ya kuchukua leo; Kauli ya kujiambia leo “chochote ninachofanya kama hakiniui basi kitaniimarisha.”
Jitie moyo na hamasa kwa kujiambia maneno ya kukushawishi kwenda hatua ya ziada. Usikubali kushindwa kuchukua hatua kwenye kile unachotaka kwenye maisha yako.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo