Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Sababu Kwa nini Unasali Halafu Hupati Kile Unachoomba?

Kila mmoja wetu huwa anasali kadiri ya imani yake. Watu wengi wanasali lakini hawapati kile wanachoomba je, umeshawahi kujiuliza ni kwa nini? Ni kwa sababu hawasali ipasavyo. Nikirejea katika kitabu cha Yakobo, kinasema haya “mnaomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu” Nina ungana mkono na Yakobo. Wengine wanaomba …

Ukitaka Kufanikiwa Cheza Na Kitu Hiki

Cheza na hisia za watu. Ukitaka ukubaliane na watu cheza na hisia za watu.Chochote unachofanya angalia na gusa hisia za watu. Binadamu ni viumbe vya hisia. Hivyo utafanya yote lakini kama hugusi hisia zao huwezi kufanikiwa kwa lolote unalotaka. Hata uchumi wa sehemu yoyote ile unapanda au kukua kadiri ya hisia za watu. Watu wakisema …

Wewe Siyo Kiranja Wa Dunia

Kuna watu ambao wanapenda kujipa kazi ambayo hata siyo yao. Kazi yenyewe ni ya kuwa kiranja wa dunia kutaka kuwanyoosha watu. Mtu anapokuwa kiranja wa dunia maana yake anataka mambo yaende kama vile anavyotaka yeye. Anataka watu waishi vile anavyotaka yeye. Ukitaka dunia iende kama vile unavyotaka wewe hiko ni kitu ambacho hakiwezekani. Unaweza kujitawala …

Mtumie Mtu Huyu Hapa Kama Umekosa Watu Wa Kukuhamasisha

Hamasa ni kichocheo kinachokufanya mtu uendelee kujisukuma na kufanya kile unachopaswa kufanya. Watu wanaweza kwenda mbele wakiwa na hamasa au kurudi nyuma sana kwa kukosa hamasa. Na binadamu ndivyo tulivyo bila hamasa hatujisukumi kufanya. Zawadi zimewekwa ili kuibua hamasa ndani yetu ya kufanya kazi kwa bidii zaidi. Ni muhimu sana hamasa katika maisha yetu ya …

Chukua Hatua Hii Hapa Pale Unapofikia Hali kama Hii

Kuna wakati unafikiria mpaka akili inachoka na kufikia ukomo.Unaona kabisa hapa siwezi kufanya kitu. Leo ninayo habari njema sana kwako. Ukifikia hali kama hiyo acha imani itawale. Acha Mungu achukue nafasi yake. Hutakiwi kujitesa kwa kila kitu na hutakiwi kufanya kila kitu peke yako. Na siyo kila kazi ni yako. Kazi zingine siyo zako ziko …

Haya Ndiyo Matokeo Ya Kutosema Ukweli Wa Mambo

Usiposema ukweli wa mambo, watu watatunga hadithi wanazojua wao. Kama familia, kikundi, taasisi au kampuni jambo linapotokea liwekeni wazi kabla watu hawajaanza kusema yale ambayo hayapo. Unapoweka ukweli hadharani, watu wanashindwa kutengeneza hadithi mpya. Lakini, ukificha mambo usipotoa taarifa watu watabaki njia panda na hapo ndipo wanaamua kusema vitu ambavyo haviko. Usisubiri mpaka watu watengeneze …

Hakuna Makubwa Bila Madogo

Ni kweli. Kila tatizo kubwa lilianza kidogo. Huwa tunakuwa tunadharau jambo dogo bila kujua baadaye linakuwa kubwa. Chunguza katika mahusiano yako yoyote yale, uliliona jambo dogo ukalidharau ukaliacha mpaka likakua kubwa. Kwa mfano, mtoto usipomlea vizuri baadaye anakuja kuwa tatizo kwa wazazi au jamii kwa ujumla. Huwa tunapata ishara mbalimbali ya vitu pale mambo yanapokuwa …

Hakikuui Bali Kinakuimarisha

Watu huwa wanalalamika juu ya vile wanavyofanya na vile wanavyofanyiwa. Unaweza ukawa unafanya kazi sana watu wakakusema na kukuambia huchoki au hujionei huruma. Usipofanya kazi watu watakuona mzembe na ukifanya kazi watu wanakuona wewe ni mtu unayejitesa. Sasa ufanye lipi? Fanya kazi. Unajua kwa nini? Kwa sababu; chochote kile unachofanya kama hakikuui basi, kinakuimarisha. Ukiwa …

Ukiwahudumia Vizuri Watu Hawa Lazima Utafanikiwa

Tumeitwa kutumika na siyo kutumikiwa. Kila mmoja anaalikwa kuwatumikia watu na siyo kutumikiwa. Yeyote unayekutana naye na anahitaji huduma kutoka kwako ukifanikiwa kumhudumia vizuri sana lazima utafanikiwa. Ukiwahudumia vizuri wale wanaohitaji huduma kutoka kwako lazima utafanikiwa. Hakuna kingine kitakachokutoa hapo ulipo kama huna huduma bora. Wale ambao wanategemea huduma kutoka kwako, hakikisha unawahudumia vizuri sana. …

Hiki Ndiyo Kitu Cha Maana Zaidi

Natumaini una ndoto, je, ndoto yako imefikia wapi? Iko kichwani au iko kwenye matendo? Huenda una ndoto na hujui namna ya kufikia ndoto yako, kama una ndoto na hujui namna ya kufikia ndoto yako, jipatie nakala ya kitabu kinachoitwa jinsi ya kufikia ndoto zako kwa mifano kilichoandikwa na Godius Rweyongeza. Kitakusaidia kupata mwongozo kwenye safari …