Ni kweli.
Kila tatizo kubwa lilianza kidogo. Huwa tunakuwa tunadharau jambo dogo bila kujua baadaye linakuwa kubwa.
Chunguza katika mahusiano yako yoyote yale, uliliona jambo dogo ukalidharau ukaliacha mpaka likakua kubwa. Kwa mfano, mtoto usipomlea vizuri baadaye anakuja kuwa tatizo kwa wazazi au jamii kwa ujumla.
Huwa tunapata ishara mbalimbali ya vitu pale mambo yanapokuwa hayapo sawa. Kwa mfano, mwili unapokuwa unashida eneo fulani unakupa ishara kua eneo fulani haliko sawa. Usipochukua hatua baadaye linakuja kuwa tatizo kubwa ambalo mwanzoni lilikuwa dogo
Hata gari likiwa linahitilafu linakuonesha ishara. Usipofunga mkanda kiashiria kinakuja na kukutaka ufunge mkanda.
Usidharau vitu vidogo. Kile ambacho umekiona kikubwa leo kilikuwa kidogo jana.
Leo nakusihi usidharau kile ambacho unacho hata kama ni kidogo. Kitumie vizuri ili kiwe kikubwa zaidi. Vitu vyote vilianzia chini hivyo tumia kile kidogo ili kizalishe kikubwa zaidi.
Ukiona tatizo dogo limejitokeza anza kulifanyia kazi haraka. Kwani ukiliacha ndiyo linakuwa tatizo kubwa baadaye.
Hatua ya kuchukua leo; Pata muda tafakari yale mambo yote madogo uliyokuwa unayadharau yalivyokuwa makubwa baadaye.
Vipi kama ungechukua hatua leo hii ungekuwa wapi? Kwa funzo ulilopata usirudie kudharau jambo dogo linapojitokeza kwenye kila eneo la maisha yako.
Chochote kile unachotaka kufanya kifanye bila kujali udogo wake.
Tibu tabia hasi ambayo hujaipenda mapema kabla haijaenea kama vile kansa.
Shughulikia tatizo dogo kabla halijawa kubwa.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo