Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukitaka Kufanikiwa Cheza Na Kitu Hiki

Cheza na hisia za watu.

Ukitaka ukubaliane na watu cheza na hisia za watu.
Chochote unachofanya angalia na gusa hisia za watu.

Binadamu ni viumbe vya hisia. Hivyo utafanya yote lakini kama hugusi hisia zao huwezi kufanikiwa kwa lolote unalotaka.

Hata uchumi wa sehemu yoyote ile unapanda au kukua kadiri ya hisia za watu. Watu wakisema kwa sasa hela ipo na hela itaonekana kweli. Ila watu wakilalamika hela ngumu na utaona mambo magumu kweli.

Hisia za watu zina nguvu kubwa za kubadili chochote kile. Kwa mfano, maeneo ya Arusha mjini yuko mtu mmoja ambaye ni kipofu huwa anauza viberiti kwa kutembeza sasa akikutana na mtu akimwambia nauza viberiti hata kama mtu hana uhitaji anajikuta ananunua tu. Kwa nini kwa sababu ya hisia tu ya jinsi alivyomuona muuzaji hisia za huruma zikamwingia na anajikuta ananunua tu.

Wewe kama ni mfanyabiashara usibishane na soko. Bali fanya kadiri soko linavyotaka. Ukibishana na soko utaumia. Nenda kadiri ya uhitaji wa soko.

Kwenye mauzo wauzie watu kile ambacho watu wanataka. Kwa kufanya hivyo ni rahisi kuuza.

Hatua ya kuchukua leo; nenda kafanye kitu kulingana na hisia za watu zinataka nini.

Mafanikio makubwa yamelala pale unapogusa hisia za watu. Fanya kitu ambacho kitaenda kugusa hisia yake moja kwa moja kiasi kwamba mtu akiamua kufanya maamuzi harudi nyuma.

Ukitaka kujua hisia zina nguvu ni hata wewe pale unapokuwa na hisia ya kufanya kazi fulani au kitu fulani utajikuta siku hiyo unafanya kazi kweli kupita hata maelezo.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: