Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Sababu Kwa nini Unasali Halafu Hupati Kile Unachoomba?

Kila mmoja wetu huwa anasali kadiri ya imani yake. Watu wengi wanasali lakini hawapati kile wanachoomba je, umeshawahi kujiuliza ni kwa nini?

Ni kwa sababu hawasali ipasavyo. Nikirejea katika kitabu cha Yakobo, kinasema haya “mnaomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu”

Nina ungana mkono na Yakobo. Wengine wanaomba wapate hitaji fulani siyo kwa lengo zuri bali baya. Wako wengine wanaomba wapate kuwa kiongozi ili waweze kujinufaisha na siyo kusaidia jamii.

Unaposali au kuomba kitu chochote chunguza kwanza je, kile unachoomba unaomba kwa nia nzuri. Kama unaomba kwa nia nzuri utakipata kweli.

Kwa mfano, siku moja nilikuwa maeneo fulani, nikakutana na vijana wawili wakiwa wanaongea. “Mmoja alimwambia mwenzake. Aisee, nina muomba Mungu anijalie nipate gari. Halafu akamalizia na kusema, yaani nikipata gari mademu watanikoma. Nitawajaza kwenye gari. “

Rafiki, umeona nia ya hao vijana hapo juu niliotolea kama mfano? Je, unafikiri kwa nia yao ya kuomba watapata kile wanachotaka?

Unapoomba upate utajiri ili uweze kuwasaidia wengine ni rahisi kupata. Kuliko kuomba utajiri kwa ajili ya kuangalia familia yako tu. Huo unakuwa ni ubinafsi.

Unapoomba kitu kwa nia mbaya ni ngumu kukipata. Asili huwa haipendi mtu anayejiangalia yeye mwenyewe bila kujali wengine.

Hatua ya kuchukua leo; unaposali kuwa mnyenyekevu, kuwa na imani na kuwa na udumifu katika sala. Kama unaomba omba bila kuchoka, ukiwa na imani na unyenyekevu.

Kwa hiyo, usiombe kwa nia mbaya ili upate kutosheleza tamaa zako. Kuwa makini sana maana tamaa zako zinaweza zikasababisha kukosa kile unachotaka kwa sababu ya kuomba au kutaka kwa nia mbaya.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: